BARAZA
la madiwani wa halmashauri ya Musoma limegawanyika kwa mara ya kwanza na
kufanya baadhi ya madiwani kutoka nje na kususia kikao baada ya
kutofatiana kimtazamo juu ya ugawaji wa halmashauri ndani ya wilaya ya
Butiama.
Tofauti
hiyo ilitokea jana wakati wa kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo ambayo makao makuu yake
bado yapo ndani ya Manispaa ya Musoma.
Baadhi ya madiwani hasa upande wa kambi
ya upinzani walikuwa wakidai kuwa wananchi wa kata ambazo zimegawanywa
na kuwa halmashauri ya Musoma hawatatendewa haki endapo watakuwa chini ya Mkuu wa wilaya ya Butiama.
Akichangia hoja hiyo diwani wa kata ya Bukima Ruti Mayamba alisema
wawo kama wawakilishi wa wananchi hawatakuwa wamewatendea haki kutoka
kata za majita na Lukuba kwani watakuwa mbali na huduma za kiutawala .
Mayamba alisema huduma zitakuwa karibu endapo watakuwa chini ya mkuu wa wilaya ya Manispaa ya Musoma.
“Tunataka kata hizi kumi na saba ziungane na kata 13 za Manispaa ya Muasoma ili kutengeneza wilaya ya Musoma”,alisema Mayamba.
Kwa upande wa madiwani wa
chama Tawala waliazimia kuwepo na halmashauri mbili ya Musoma na
Butiama ndani ya wilaya ya Butiama ambazo zitakuwa chini ya Mkuu wa
wilaya hiyo ya Butiama.
No comments:
Post a Comment