Na Mwandishi wetu
Bonanza
la michezo la nane nane soccer bonanza lililokuwa lifanyike siku ya
tarehe 8 mwezi wa 8 katika viwanja vya Tanganyika perkasi vilivyopo kawe
jijini Dar es Salaam limesogezwa mbelea kwa ajili ya kupisha mwezi
mtukufu wa ramadhani.
Bonanza
hilo litakaloshirikisha timu mbalimbali za mpira wa miguu, mpira wa
mikono ( valleyball ) na michezo mingine mingi sasa linatarajiwa
kufanyika baada hiki kipindi cha mfungo mwezi wa ramadhani kuisha.
Salum
Suleiman (pichani), ambaye ndio mratibu wa bonanza hilo aliyasema hayo
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za
waandaaji wa bonanza hilo, SULE'S INC & ENTERTAINMENT zilizopo kawe jijini Dar es Salaam.
Suleiman
amesema wamefikia uamuzi wa kalisogeza mbele bonanza hilo kutokana na
maoni mengi ya wadau wa soka ikiwa ni pamoja na baadhi ya timu
zitakazoshiriki bonanzna hilo kuomba kusogezwa mbele. "maoni mengi ya
wadau na hata baadhi ya timu shiriki yamekua yakisisitiza kuomba
kusogeza mbele bonaza hilo kwa sababu kupisha mwezi mtukufu wa
Ramadhani"
Aidha
suleiman aliongeza kuwa maandalizi ya bonanza hili yalikuwa
yamekamilika kwa asilimia kubwa ila kamati yake imefikia uamuzi wa
kulisogeza mbele kutokana na kuheshimu mawazo ya wadau na hata wachezaji
wenyewe "napenda kuishukuru kamati ya maandalizi ya Nane nane Soccer
Bonanza kwani imeweza kukamilisha sehemu kubwa ya maandalizi ya bonanza
hili ila kutokana na kuheshimu mawazo na maoni ya wadau walio wengi
tumeamua kulisogeza mbele bonanza letu mpaka hapo mwezi wa ramadhani
utakapomalizika"
No comments:
Post a Comment