Mabondia
Mussa Sunga kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakioneshana
umwamba wa kutupiana masumbwi wakati wa mazoezi yao ya kujitaalisha na
mapambano ya ngumi siku ya Idi pili Sunga atacheza na Mussa Seifu 'Boda
boda katika uwanja wa Bandari na Class atapambana na Sako Mwaisege
'Dunga' katika ukumbi wa Diamond Juble
KAMBI YA NGUMI ya Ilala jijini Dar es
salaam ipo katika mazoezi ya kuwaandaa mabondia wake wawili watakaopanda
ulingoni siku ya Iddi pili katika viwanja viwili tofauti
Akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi anaesimamia Kambi ya Ilala Rajabu Mhamila 'Super D'
amesema kuwa mabondia hawo Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Mussa Sunga
aliongeza kwa kusema kuwa mpambano wa
Sunga litafanyika katika uwanja wa Bandari Tandika Dar es salaam na
atazichapa na Mussa Seif 'Boda Boda' siku ya Idd pili
na bondia Class atapanda ulingoni siku hiyo hiyo katika ukumbi wa Diamond Jublee kuzipiga na bondia Sako Mwaisege 'Dunga'
aliongeza kwa kusema mabondia hawo wapo
katika mazoezo mazito wakisimamiwa na yeye mwenyewe na kocha mkongwe wa
mchezo huo Habibu Kinyogoli 'Masta' pamoja na Kondo Nassoro
Katika michezo hiyo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi
pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na
kocha wa mchezo huo, Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya
kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za
masumbwi.
Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo
yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia, makocha waamuzi
pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.
''Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd
Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na Mtanzania Roja Mtagwa
anayefanya shughuli zake Marekani.
“DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari katika mchezo huo wanatakiwa
kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi,''
alisema Super D. DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara
ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi Ilala na klabu ya Ashanti
ya Ilala hapa Jijini. |
No comments:
Post a Comment