Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 2, 2012

MAHAKA YA KAZI YAAMURU WALIMU KURUDI KAZINI MARA MOJA


Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Gratian Mkoba, akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi aliofuatana nao kwenye kusikiliza maamuzi ya kesi iliyofunguliwa na serikali kwenye Mahakama Kuu Divisheni ya biashara kupinga mgomo ulioitishwa na Chama hicho ambao umeanza tangu juma tatu wiki hii. Mhakama imewaamuru walimu kurejea kazini mara moja.
Katibu Mkuu wa CWT Mwl. Ezekiel Oluoch akiondoka kwenye Mahaka Kuu Divisheni ya Kazi mara baada ya kusikiliza Hukumu ya Kesi iliyofunguliwa na serikali dhidi ya Chama hicho kufuatia kuitisha mgomo wa walimu nchi nzima wakidai nyongeza ya mishahara kwa asilimia 100.
Baadhi ya watu waliojitokeza kusikiliza hukumu hiyo wakiwemo, walimu, waandishi wa habari na wadau wengine wa sekta ya elimu wakiondoka mara baada ya kusomwa hukumu.
MAHAKAMA Kuu Divisheni ya kazi ya jijini Dar es Salaam leo imewaamuru walimu kurudi kazini maramoja kutokana na mgomo wanaoundesha kukosa uhalali. Akisoma hukumu hiyo hakimu anae sikiliza kesi hiyo jijini Dar es Salaam leo alisema taarifa iliyotolewa kwa mwajiri ya masaa 48 ilifanya kazi kwa muda usiozidi saa 1:30 kutokana na kutolewa siku ya ijumaa saa tisa mchana huku ikizingatiwa siku za jumamosi na jumapili sio siku za kazi.


Sababu nyingine iliyotosha kuharamisha mgomo huo ni namna upigaji kura ulivyoendeshwa umekua wautatanishi lakini mbali na kura zenyewe hata barua iliyotoa taarifa ya kuwepo kwa upigaji kura haikueleza kupiga kura ya kuunga mkono mgomo bali ilieleza kuunga mkono madai ya walimu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...