Kariati akizungumza neno la kufungua shughuli. Kulia ni Mama Nyerere
Kisha Kariati akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Nyerere kama shukurani ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa Mwalimu mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo.
Halafu akamkabidhi mkoba wa safari kama akitaka kwenda Butiama
Mama Nyerere akapata fursa ya kuzungumza mambo mbalimbali kabla ya kukabidhi trekta kwa wakulima hao, ambao pichani wamekaa kushoto.
Mama Maria Nyerere na Kariati wakaongozana na wakulima kwenda eneo la makabidhiano ya trekta
"Trekta zenyewe ndiyo hizi" akasema Kariati kumwambia Mama maria Nyerere
Mama Maria akimkabidhia funguo za trekta moja kati ya kumi aliyokabidhi, mmoja wa wakulima hao Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni Sheikh wa Kata ya Kwadelo.
Baadha ya Sheikh akamkabidhi pia mkulima Maulidi Msema funguo za trekta
Baada ya Mama Nyerere kukabidhi trekta kumi, Kariati akamshukuru
Kisha Mama Nyerere na diwani Kariati wakapigwa picha ya pamoja kuhitimisha shughuli
" UFOO SARO PIA YUPO!" akasema Mama Maria Nyerere na kupigapicha naye kwa niaba ya waandishi wote waliokwenda kwenye shughuli hiyo.
No comments:
Post a Comment