Mechi
za michuano ya BancABC SUP8R inayoshirikisha timu nane bora kutoka
Tanzania Bara na Zanzibar zinaendelea kesho (Agosti9 mwaka huu) kwenye
miji ya Dar es Salaam, Moshi, Mwanza na Zanzibar.
Mkurugenzi
wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Saad
Kawemba na viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) chini ya
Rais wao Amani Makungu walikutana leo mjini Zanzibar kuzungumzia
maendeleo ya michuano hiyo. Viongozi wengine wa ZFA waliohudhuria kikao
hicho ni Katibu Mkuu Kassim Haji Salum na wajumbe saba wa Kamati ya
Utendaji.
Katika
kundi A Jamhuri itacheza na Zimamoto kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar
kuanzia saa 2 kamili usiku, wakati Simba itaparurana na Mtende kwenye
Uwanja wa Ushirika, mjini Moshi. Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni.
Azam
itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es
Salaam wakati Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza utakuwa mwenyeji wa
mechi ya Polisi Morogoro na Super Falcon. Mechi hizo zote za kundi B
zitaanza saa 10 kamili jioni.
Hatua
hiyo ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu kwa mechi nne. Simba na
Zimamoto zitaoneshana kazi Uwanja wa CCM Kirumba wakati Jamhuri na
Mtende zitacheza kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi
za kundi B zitakuwa kati ya Super Falcon na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja
wa Amaan na Azam dhidi ya Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Ushirika.
|
Marquee
tangazo
Wednesday, August 8, 2012
MECHI ZA MICHUANO YA BancABC SUP8R KUENDELEA KESHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment