Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 13, 2012

MSAMA AUCTION MART YASHIRIKIANA NA CHAMA CHA FILAMU TANZANIA KATIKA ZOEZI LA KUKAMATA WEZI WA KAZI ZA WASANII


Viongozi wa Chama cha Filamu Tanzania wakiwa kikao cha kujadili namna ya kupambana na maharamia wa kazi za wasanii nchini. Wa tatu kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama  akiwa kwenye kikao cha pamoja na wadau wa Chama cha Filamu Tanzania (TAFF), mwishoni mwa wiki kujadili na kupanga mikakati dhidi ya vita hiyo inayolenga kupigania mafanikio ya wasanii.  
 Mwenyekiti wa Bongo move Jacob Stevin 'JB' kushoto akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam juu ya wizi mkubwa uliotokea hivi karibuni uliofanywa na Kampuni ya Steps Entatainmenti kwa kushirikiana na wasanii wenyewe na kudai kuwa tabia hii ikomeshwa kwa maharamia wa kazi za wasanii. Kulia ni Msanii Vicent Kigos 'Ray' na Mwenyekiti wa Shilikisho la Filamu Tanzania 'TAFF' Simon m Mwakifwamba
 Viongozi wa Chama cha Filamu Tanzania TAFF wakionesha kazi Feki za wasanii walizokamata hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama akionyesha CD na DVD feki zenye thamani ya sh. milioni 11 zilizokamatwa katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam, wakati wa operesheni ya kuwakata wezi wa kazi za wasanii inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi. 
Mwasisi wa kampeni ya kupambana na maharamia wa kazi za wasanii nchini, Alex Msama (wa pili kushoto) akiwa kwenye kikao cha pamoja na wadau wa Chama cha Filamu Tanzania (TAFF), mwishoni mwa wiki kujadili na kupanga mikakati dhidi ya vita hiyo inayolenga kupigania mafanikio ya wasanii.
Alex Msama akionesha CD Feki pamoja na DVD walizokamata katika maeneo ya Mbagala.
Mashine za Kurudufu kazi Feki za wasanii.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...