Na Mwandishi Wetu
Bendi
zenye upinzani wa jadi nchini kama ule wa Simba na Yanga, Msondo Ngoma
Music Band na Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae)
zitapambana siku ya Iddi Mosi kwenye viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni.
Tayari
mashabiki wa bendi hizo wameanza maandalizi ya kuzishangilia bendi zao.
Mpambano huo umeandaliwa na kampuni za Keen Arts na kudhaminiwa na
kinywaji cha Konyagi.
Mratibu
wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la
kusherekea sikukuu ya Iddi na kuamua ni bendi gani bora kati ya magwiji
hao wawili wa muziki wa dansi nchini kwa mwaka 2012.
Kapinga
alisema ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa, kila bendi itatumia jukwaa
lake kwa kupiga kwa muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda jukwani.
“Litakuwa
pamabano la aina yake ukizingatia kuwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa
bendi hizi pinzani kupambana siku ya sikukuu ya Iddi tangu zianzishwe”
alisema Kapinga. “Pia itakuwa ni mara ya kwanza kwao kushindana katika
viwanja vya Leaders Club.”
Kapinga
alisema kampuni yake inafanya mipango ya kuwasafirisha wapenzi wa bendi
hizo kutoka kila wilaya ya Dar es Salaam kuja kushuhudia mpambano
huo.Alisema mchuano huo itaanza saa nane mchana hadi liamba.
Mwaka
jana bendi hizo zilipambana vikali kwenye ukumbi wa TCC Club sikukuu ya
Krismasi ambapo mbali na muziki safi na vituko vya hapa na pale kama
ilivyo kawaida, zilitoka sare kwa kupata pointi sawa.
Mratibu amesema kuwa mwaka huu mshindi ni lazima apatikane hata kwa kurusha shilingi.
No comments:
Post a Comment