Kada wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM), Daud Msungu (kushoto), akirejesha fomu za kuomba kugombea nafasi ya
makamu mwenyekiti wa umoja huo, kwa Sophia Duma ambaye ni Mkuu wa Idara ya
Organaizesheni Makao Makuu ya UVCCM, Dar es Salaam jana. Msungu alikuwa mjumbe
wa Baraza la umoja huo kupitia Mkoa wa Lindi.
Msungu akionesha fomu alizozirejesha
Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kurejesha fomu hizo, Msungu, alisema endapo akifanikiwa kugombea na kushinda wadhifa huo, atamshauri mwenyekiti, kuweka mikakati ya kuwashawishi vijana kushiriki katika ujenzi wa uchumi na maendeleo ya Taifa, kwa vile vijana ndiyo nguvu ya Taifa.
Pia amesema kuwa, atahakikisha wanarudisha umoja na mshikamano kwa vijana kwa ajili ya ustawi wa Chama Cha Mapinduzi.
"Hiyo itasaidia vijana kusukuma mbele, gurudumu la maendeleo ya Taifa letu, kuendana na kasi ya kiuchumi na maendeleo hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kiuchumi yanayoendelea duniani" alisema Msungu.
Atashirikiana na viongozi wengine wa umoja huo, kuandaa mipango ya mafunzo kwa vijana kuielewa vizuri itikadi ya chama, hasa kwa kufufua vyuo mbalimbali vya itikadi ikiwemo Kambi ya Ihemi, mkoani Iringa..

No comments:
Post a Comment