LONDON, England
Aguero,
aliyefunga mabao 30 katika msimu wake wa kwanza katika soka la England,
anaamini nyota wa Man City wamethibitisha kuwa hawakamatiki katika mechi
ya Ngao ya Jamii waliyoshinda dhidi ya Blues
SIKU chache kabla ya kuanza kwa smimu mpya
wa Ligi Kuu ya England, mshambuliaji Sergio Aguero anaamini mabingwa
watetezi wa ligi hiyo Manchester City, wako tayari kuzima matarajio ya
majirani zao kwa mara nyingine.
Muargentina
huyo alifunga dakika ya mwisho kuipa City ubingwa huo msimu uliopita,
huku akizima matarajio ya mshambuliaji Wayne Rooney na kikosi chake caha
Manchester United.
Na kuelekea pambano la
juzi la Ngao ya Jamii kati ya City na Chelsea, Rooney aliyefunga jumla
ya mabao 35 ya michuano ya ndani msimu uliopita alikaririwa akiionya
City kuwa hatima ya mwisho ya ubingwa wa msimu huu iko mikononi mwa
United.
Lakini Aguero, ambaye alifunga jumla
ya mabao 30 katika msimu wake wa kwanza wa kuvutia katika soka la
England, anaamini nyota wenza kikosini Etihad wamethibitisha uhatari wao
katika mechi ya Ngao ya Jamii waliyoshinda dhidi ya Blues.
“Tumefanya mwamzo mwema wa msimu na wiki hii tunaingia katika mechi yetu ya kwanza ya utetezi wa taji letu.
“Tumeanza
kupiga hatua juu ya wengine na tuna matumaini kuwa Mungu atataubaklisha
katika kiwango na morali tuliyonayo kama hivi. Tumekuwa timu imara na
tumeanza kuelewana zaidi ya ilivyokuwa.
“Tutajaribu
kuanza kama ilivyokuwa msimu uliopita na kufanya mambo vema zaidi.
Nimekuwa nikiomba na kujiona kama tunaoweza kufanya hivyo tena. Sitaki
kusema kwamba msimu utakuwa rahisi, lakini tuna timu nzuri ya kufanya
hivyo.”
Aguero alijiandikia jina katioka
historia ya City, kufuatia bao tamu la dakika za majeruhi kuipa ushindi
uliowatawaza mabingwa baada ya miaka 44 katika siku ya kufunga msimu
dhidi ya QPR.
Lakini sasa Aguero anasisitiza
kuwa, huo ulikuwa mwanzo tu: “Mimi nilielewa siku ya pili kile
nilichofanya dhidi ya QPR. Lakini sasa kwambaaa nina imani kubwa na
matumaini kuwa City inaweza kushinda zaidi,” alimaliza Aguero katika
tambo zake.
No comments:
Post a Comment