Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) ambaye pia ni Mkaguzi wa
hesabu za Umoja wa Mataifa (UN) Ludovick Utouh akiongea na waandishi wa
habari kuhusu Taasisi
10 za UN ambazo zitafanyiwa ukaguzi chini ya usimamizi wake ambapo
watumishi 60 kutoka ofisini yake watafanya kazi hiyo. Kwa kipindi cha
miaka sita nchi za Tanzania, China na Uingereza zimepewa jukumu la
ukaguzi wa hesabu za UN.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Edwin Rweyumamu kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za
Serikali (CAG) akimkaribisha
CAG ambaye pia ni Mkaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa (UN) Ludovick
Utouh ili aweze kuongea na waandishi wa habari kuhusu Tanzania kupata
nafasi ya kukagua hesabu za UN kwa kipindi cha miaka sita. Watumishi 60
kutoka ofisi ya CAG watafanya kazi ya kuzikagua taasisi 10 za UN.
No comments:
Post a Comment