Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Silabu, Mizeki Charahani akiwa ofisini kwake
Baadhi ya Wanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Silabu wakiwa darasani kwao. (Picha na mtandao wa Thehabari.com)
Na Joachim Mushi, Korogwe
Baadhi ya Wanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Silabu wakiwa darasani kwao. (Picha na mtandao wa Thehabari.com)
Na Joachim Mushi, Korogwe
WANAFUNZI wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Silabu
iliyopo Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga wanasomea kwenye uchochoro
unaotenganisha kati ya darasa moja na lingine kutokana na uhaba wa vyumba vya
madarasa.
Wanafunzi hao ambao darasa lao limekuwa likihama kila muda
kutengemea hali ya hewa (jua na mvua) kufuata kivuli wamelazimika kusomea nje
kwenye uchochoro ambao haujaezekwa kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni
hapo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni katika
shule hiyo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Silabu, Mizeki Charahani alisema
wanafunzi hao wamelazimika kusomea nje kwa kuwa wanavyumba vinne tu vya
madarasa ambavyo havitoshelezi kwa mahitaji ya shule.
Akifafanua zaidi alisema darasa hilo eneo lao maalumu la kusomea (darasa) ni
kwenye uchochoro unaotenganisha kati ya darasa moja na lingine, lakini huwa
wanahama jua linapozidi au mvua kunyesha na kwenda eneo lingine linalokuwa na
kivuli.
“Darasa hili kwa kweli huwa linahama kulingana na hali ya
hewa, jua likizidi wanabeba madawati yao
na kuhamia eneo lenye kivuli, mvua ikinyesa hivyo hivyo wanahamia sehemu
nyingine…lakini muda mwingine tunawahamishia kwenye darasa moja na wenzao pale
kunapokuwa hakuna mwingiliano wa vipindi,” alisema Charahani.
Alisema shule hiyo yenye darasa la kwanza hadi la saba unauhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa kwani hata darasa la kwanza na la pili wanasomea kwenye darasa moja kwa kupokezana.
“Kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa hata hatuna darasa
la awali wala ofisi ya walimu…na sisi ofisi yetu ipo hapa chini ya mti huu,”
alisema Mwalimu huyo huku akionesha eneo moja chini ya mti ulio mbele ya
madarasa ya shule hiyo.
Akizungumzia hali hiyo, Ofisa Elimu Taaluma, Halmashauri ya
Mji wa Korogwe, Elius Mkwizu alikiri kuwepo kwa tatizo hilo la uhaba wa vyumba vya madarasa katika
shule hiyo na kudai shule hiyo ni mpya hivyo ujenzi wake haukwenda sambamba na
ongezeko la wanafunzi kimadarasa.
Alisema tayari uongozi wa idara hiyo kwa kushirikiana na
wananchi unafanya ujenzi wa madarasa mawili ambayo yatasaidia kupunguza uhaba
wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo. Hata hivyo aliongeza ujenzi huo kwa
sasa umesimama baada ya fedha zilizotengwa kurejeshwa hazina kuu baada ya kukaa
kipindi kirefu bila kutumiwa.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia moja ya ujenzi wa
darasa lililosimama baada ya kukosekana kwa fedha za kuliendeleaza. Akifafanua
zaidi Mkwizu alisema kulikuwa na mvutano kati ya viongozi waliokuwawakisimamia
ujenzi huo na wananchi hali iliozua mgogoro na ujenzi kusimama.
No comments:
Post a Comment