Na Zawadi Msalla – Maelezo, Dodoma
SERIKALI inaandaa mpango madhubuti wa
ulipaji pensheni kwa wazee kote nchini ili kuboresha maisha yao jambo
ambalo litawafanya waishi maisha marefu zaidi.
Akijibu swali la nyongeza lililoulizwa bungeni leo, Waziri wa Kazi na Ajira Gaudencia Kabaka alisema kuwa wizara yake imeandaa utaratibu utakaowasaidia wazee kulipwa pensheni kuanzia mwaka 2013.
Akijibu swali la nyongeza lililoulizwa bungeni leo, Waziri wa Kazi na Ajira Gaudencia Kabaka alisema kuwa wizara yake imeandaa utaratibu utakaowasaidia wazee kulipwa pensheni kuanzia mwaka 2013.
Utoaji wa pensheni hiyo utaenda sambamba na uanzishwaji wa sheria mpya ya wazee inayotarajiwa kuanza kutumika mwaka 2013.
Awali akijibu swali la msingi Naibu Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid alisema kuwa sheria hiyo
imejikita zaidi kutetea haki za wazee na kuboresha maisha yao kwa
kuhakikisha kuwa wanatambuliwa na kupewa fursa ya kushiriki kwenye
mambo yanayohusu maisha yao ya kila siku kwa manufaa ya watanzania wote.
“Wizara imekuwa ikishughulikia upatikanaji
wa sheria hiyo, rasimu ilishaandaliwa na kujadiliwa na wadau kwa hivi
sasa inafanyiwa maboresho ili iwasilishwe katika ngazi ya sekretariet.”
Alisema Dk. Seif.
Zoezi la kuandaa sheria hiyo linafanyika kwa
awamu ambapo Serikali itawasilisha Bungeni mswada huo wa sheria mwezi
Aprili mwaka 2013.
Hata hivyo kumekuwepo na malalamiko
mbalimbali kwa ucheleweshaji wa sheria hiyo ambayo kwa sasa haki za
msingi za wazee hazipewi kipaumbele zikiwezo za huduma za afya na
maendeleo ya kila siku.
Akichangia mjadala huo Mbunge wa Viti
Maalum Magret Mkanga alishangazwa na ucheleweshwaji wa uanzishwaji wa
sheria hiyo kwani sera ya Taifa ya Wazee ilipitishwa mwaka 2003.
“Sera ya Taifa ya Wazee ilipitishwa mwaka
2003 hadi sasa miaka kumi imeshapita bado sheria haijaundwa, jambo hili
linawafanya wazee wapate huduma kwa huruma tu”, alisema.
No comments:
Post a Comment