Beki
wa timu ya APR ya Rwanda, Mbuyu Twite, aliyesaini Klabu ya Yanga ya
jijini Dar es Salaam, akiweka Dole katika karatasi zake na mkataba
baada ya kumwaga wino na Klabu hiyo leo na kuwaacha mjia panda Viongozi
wa Simba, ambao tayari walikwisha tangaza kumsajili na kumtambulisha
rasmi katika Siku maalu ya Simba 'Simba Day' na kutambulisha jezi No, 4
kuwa ndiyo ingekuwa jezi ya Beki huyo, jambo ambalo limeonekana na
kujulikana ukweli leo hii baada ya mchezaji huyo kuweka mambo
hadharaniu. Picha na Michuzi Blog
Mbuyu Twite, akisaini mkataba wake na timu ya Yanga, le.
Beki
wa timu ya APR ya Rwanda, Mbuyi Twite, aliyesaini Klabu ya Yanga ya
jijini Dar es Salaam, akikabidhiwa jezi yake mpya na Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Binkrebu, leo wakati wa hafla fupi ya
kumsainisha.
******************************
IKIWA
ni siku moja tu baada ya Mwenyekiti wa Simba Ismail Rage, kutoa
malalamiko kuwa wanachezewa rafu na Mahasimu wao Yamga na kumtuhumu
mtoto wa kigogo kuhusika kuwahujumu katika usajili wa beki wa Rwanda
Mbuyu Twite, uongozi wa Yanga umekuja juu na kumtaka Rage adhibitishe
kauli yake ikiwa ni pamoja na kumtaja mtoto huyo wa kigogo.
Yanga
wamefanya kweli kwa kuweka wazi suala la mchezaji huyo na kumsainisha
na kuwaacha Mahasimu wao midomo wazi wasijue la kufanya juu ya Beki huyo
baada ya Yanga kukamilisha taratibu zote za uhamisho wa kimataifa wa
Beki huyo na kufuata taratibu.
Rage
alitoa kauli hiyo juzi mpaka kumpelekea kumwaga chozi sambamba na
kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati ya
Katiba,Sheria,Maadili na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kwa madai ya shirikisho hilo kuikandamiza klabu yake.
Akizungumza
na waandishi Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Twiga na Jangwani Katibu
Mkuu Yanga,Selestine Mwesigwa, alisema kuwa wao wanajua Rage ni
muugwana na ni mkubwa katika nchi hii wanajua atamtaja na kuleta
vithibitisho juu ya hilo mapema bila ya kuambiwa muda.
Aidha
Mwesigwa alitoa ufafanuzi juu ya suala la mchezaji Mbuyu Twite ambaye
inasemekana Simba wamemsajili na kusema kuwa wao Yanga wamemsajili kwa
kufuata na kuheshimu kanuni na sheria za Cuf,TFF na FIFA hivyo basi wao
hawajakurupuka katika usajili wake.
“Wenzetu
naweza sema wamekurupuka kwa kuwa hawajafuata sheria wakati ndugu yangu
Rage anajua kanuni na Sheria kwa hili namshangaa sana.”alisema
Mwesigwa.
Alisema
wao wameanza kufanya mchakato wa kumnasa beki huyo toka Novemba mwaka
jana kabla ya kuanza mazungumzo na Simba juu ya aliyekuwa beki wao
Kelvin Yondan na kusema kuwa walimtuma Mjumbe wa kamati ya Utendaji
Abdallah Binkrebu kumfuatilia toka kipindi hicho.
“Sisi
huyu mchezaji tumemsaka toka muda mrefu kabla hata ya Kagame kuanza na
mara baada ya kumalizika kwa Kagame tulikuwa tunaangalia kiwango chake
na kikaturisha.
"Binkrebu
akafunga safari na kwenda kuzungumza na uongozi wa timu yake ya Fc
Lupopo ya Kongo na wala sio APR, Simba wao wamenunua mali ya wizi wakati
sisi tumeenda kwa mwenye mali.
Aliongeza
kuwa mara baada ya leo kupeleka majina ya timu yao TFF ndipo wataweka
adharani mambo mbalimbali juu ya beki huyo ikiwa na mkataba wake wa
kuitumikia klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment