Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 14, 2014

DALADALA ZINAZOELEKEA CHUO KIKUU CHA UDOM ZAGOMA KWA SAA NNE(4)


 Wakazi wa maeneo ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa wamejazana katika kituo cha Daladala cha Jamatini mjini hapa wasijue cha kufanya baada ya Madereva wa Magari hayo kugoma kwenda njia hiyo wakishinikiza kusimamisha abiria wanapopakia.
 Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwaza jinsi ya kusafiri
mpaka maeneo ya Makulu, Chimwaga na Ng'ong'onha baada ya wenye Daladala
kugoma kutokana na kile walichodai ni kukamatwa mara kwa mara na polisi
wa usalama barabarani wakitakiwa kutojaza kupita kiasi.


Magari yanayosafirisha abiria yakiwa yameegeshwa pembezoni ya Bohari ya mkoa baada  ya madereva wa magari hayo kugoma  kutoa huduma ya usafiri kwa njia ya UDOM kwa madai ya kuonewa na Askari wa barabarani mara kwa mara katika njia hiyo japo Kamanda wa Polisi Usalma Barabarani  Boniventura Nsokolo kudai polisi hawatashindwa kuwakamata kama watawaona wakivunja sheria.
 Wanafunzi hao wakaamua kutumia usafiri wa pikipiki baada ya kuona mambo ni magumu huku wakishikiza kuwavaa wahusika.

 Na John Banda, Dodoma

MADEREVA wa Daladala zinazoenda Chuo Kikuu cha Dodoma [UDOM] manispaa ya Dodoma leo wamegoma kutoa huduma hiyo kwa zaidi ya saa 4 hali iliyosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.

Mgomo huo ulioanza majira ya saa 7 mchana ulianza kama mdhaha tu mara baada ya abiria waliokuwa katika kituo hicho kujiuliza maswali yasiyo na majibu baada ya kuona makonda wa Daladala hizo wakikufunga milango na kuwakataza wasiingie na kama haitoshi wakaamuru madereva wao wayaondoe kituoni hapo.


Madereva hao ambao walipoyaondoa magari waliyapeleka kuyaegesha maaneo ya Bohari walisema waliamua kufanya hivyo kutokana na kusumbuliwa mara kwa mara na polisi wa usarama barabarani kutokana na kusimamisha abiria.

Walisema wanashangazwa na kitendo hicho kinachofanyika na polisi wa Dodoma pekee kinyume na mikoa kama ya Mwanza, Arusha, Mbeya na hata Dar es laam ambako wanapakia watakavyo na hakuna wa kuwauliza.

Waliongeza kuwa vitendo hivyo wanavyofanyiwa vya kuzuiliwa kusimamisha abiria ni kuwatia hasara kutokana na kukosa abiria pindi wanapokuwa wakitokea UDOM ilihali sehemu yenyewe ni mbali huku mafuta yakiwa juu.

Kwa upande wake Mkuu wa polisi wa usalama Barabarani Wilaya Boniventura Nsokolo alisema kila Dereva aangalie leseni yake inamruhusu kupakikia kiasi gani, na wao kama polisi hawawezikuona Dereva akivunja sheria harafu wakamuacha bila kumchukulia hatua.

''Lazima tuwakamate kama wakivunja sheria za Barabarani kwani kila mtu ana leseni na inamuongoza apakie abiria wanagapi na kwenye kila mkoa kuna utaratibu kutokana na kitengo husika kinachosimamia na kutoa leseni hivyo ni vizuri kufuata utaratibu'', alisema Nsokolo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...