Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 14, 2014

MIYEYUSHO KUZIPIGA NA MUDDY MATUMLA APRIL 26


Promota Ally Mwazoa katikati akiwatambulisha mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakati wa kutangaza mpambano wao utakaofanyika April 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakikumbatiana baada ya kukubaliana kuzipiga April 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Miyeyusho wakitunishiana misuli na Mohamed Matumla wakati wa utambulisho wa mpambano wao mbele ya waandishi wa habari Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' na Mohamed Matumla 'Snake JR' leo wamesaini mkataba wa kupambana april 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba 

Akizungumzia mpambano huo promota wa mchezo wa masumbwi nchini Ally Mwazoa amesema ameingia nao mkataba mabondia hawo kwa kuwa anajua wanaweza mchezo wa masumbwi na ni mafundi wa mchezo huo najua kuna watu wengi walitamani kudhamini mchezo huo lakini bahati imeniangukia mie

mpambano uho utakaopigwa april 26 katika ukumbi wa pta sabasaba kutakuwa na mapambano mengine makali ya utangulizi ambapo mwana dada Lulu Kayage atamvaana na Halima Ramadhani siku hiyo kwa ajili ya kuhamasisha wanawake wenzao wajitokeze katika mchezo wa masumbwi

baada ya kusaini mkataba huo bondia Miyeyusho alijitamba kuendeleza ubabe katika familia hiyo ambapo alisema atamchakaza kama alivyo mchakaza baba yake mdogo Mbwana Matumla ambaye amecheza nae mara tatu na kupigwa mara mbili ambapo mpambano wa mwisho ulikuwa na shamu shamu nyingi kila upande miyeyeyusho alibuka mshindi kwa point

nae Matumla alijibu mapigo kwa kusema Miyeyusho anamuheshimu kwa kuwa yeyey ni mkubwa kiumri ata hivyo atampa kichapo kikali kama alivyompatia mdogo wake Doi Miyeyusho ambaye mara ya kwaza alipigwa kwa K,O raundi ya pili DDC Keko na mara ya pili pia K,O ya raundi ya pili katika ukumbi uho uho uho wa PTA Sabasaba hivyo siwezi kushusha rekodi yangu kwa kupigwa na miyeyusho akitaka kujua mimi ni mkali zaidi yao amulize pia Nassibu Ramadhani ambaye nilimpatia kipigo kibaya sana na kunifanya ninyakue pikipiki ,            Mwazoa

aliongeza kuwa ulizi na usalama wa mali zako ni wa huwakika hivyo familia nzima mnaweza kuja kushudia mpambano huo wa masumbwi bila shaka 

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...