Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, March 26, 2014

MABONDIA KUPIMA UZITO IJUMAAMabondia wanaotegemea kupigana jumamosi kugombea ubingwa wa UBO international katika ukumbi wa Karume zamani PTA hall, wakiongozwa na Thomas Mashali na Japhet kaseba wanategemea kupima uzito  siku ya ijumaa katika  hotel ya National hotel iliyopo maeneo ya keko kuanzia saa tatu asubuhi. Akizungumza na wanahabari hizi bw Ibrahim kamwe amesema kuwa mabondia wote wanaocheza mapambano ya utangulizi wapo katika hali nzuri na wale mabondia  wa mikoani wanategemea kuingia kesho alhamis wakiongozwa na alan kamote atakaecheza pambano la ubingwa wa Africa dhidi ya karage suba ambae amekuwa mbadala wa bondia fadhili awadh aliyefariki kwa ugonjwa wa malaria kali iliyomkuta kipindi akijiandaa na mapambano haya ya ubingwa, mapambano mengine yatakayopigwa siku hiyo yatakuwa kama ifuatavyo fredy sayuni motto wa keko atazipiga na Rajab mahoja wa tanga kugombe ubingwa wa taifa wa PST mabondia hawa walishawahi kuzipiga mkwakwani tanga na sayuni kuchezea kichapo kikali, safari hii Fredy sayuni anakutana nae tena kwao akitaka kulipa kisasi. Baina Mazola wa mzazi atapambana na Bakari dunda, huku dogo anayekuja juu kwa kasi na wengi humpenda kwa staili ya uchezaji wake Issa omar Nampepeche au “peche boy” atapimana ubavu na bondia mkongwe bingwa wa bantam Zuberi kitandula pia kutakuwepo na mapambano mengine mengi tu pamoja na lile la juma fundi na haji juma, shaban mtengela na jumanne Mohamed, jocky hamis na said chaku pambano la wakongwe hili .nao watakuja kupima afya zao na uzito kwa mara ya mwisho wakisubiri hukumu ya ulingoni

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...