Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, March 23, 2014

RIDHIWANI KIKWETE AHANI MSIBA WA WATOTO WAWILI WALIOPOTEZA MAISHA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI,KIWANGWA


 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) akiwa na Bw. Geofrey Nestory pamoja na Mkewe,Renata Pascal ambao ni Wazazi wa Watoto wawili,Jesca Geofrey (5) na Redempta Geofrey (2) waliopoteza maisha hivi karibuni kwa kutumbukia kwenye kisima cha maji,wakati alipofika Nyumbani kwa wazazi hao ambao ni Wakazi wa Kijiji cha Msinune,Kata ya Kiwangwa leo Machi 22,2014 kuhani msiba wa Watoto hao.Wazazi hao walimueleza Ndg. Ridhiwani Kikwete kuwa walibaini kupotea kwa watoto hao mnamo tarehe 18 Machi wakati wa jioni baada ya kuona hawajarudi nyumbani,hivyo walianza kuwatafuta na kubaini kuwa walipoteza maisha baada kutumbukia kwenye kisima hicho cha maji.Watoto hao walizikwa siku ya pili yake tarehe 19 Machi,Shambani kwao.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa amesimama kutoa pole kwa Wazazi wa Watoto hao pamoja na Waombolezaji Wengine waliokuwepo msibani hapo,kwenye Kijiji cha Msinune,Kata ya Kiwangwa leo Machi 22,2014.
Meneja wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Steven Kazidi akitoa pole kwa niaba ya CCM kwa Watoto wawili,Jesca Geofrey (5) na Redempta Geofrey (2) waliopoteza maisha hivi karibuni kwa kutumbukia kwenye kisima cha maji,wakati walipofika Nyumbani kwa Wazazi hao kuhani msiba huo Machi 22,2014.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...