Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, March 17, 2014

Evander mbabe aliyepotezaumaarufu wa TysonDVD YA HOLYFIELD VS TYSON

LEO katika maisha ya wenze
tu tutakuwa na mbabe Evander Holyfield ‘The Real Deal’ aliyeweka historia ya kuwa miongoni mwa wababe waliofanikisha kufuta rekodi ya utawala wa Mike Tyson katika ulingo.  
Mbabe huyo alishangaza dunia kwa kuweka rekodi hiyo ya kumchapa Tyson aliyekuwa anaonekana kama bondia asiyekuwa na mpinzani.
Evander akafanikiwa kuweka rekodi nyingine kwenye pambano la marudiano kwa kumpatia kichapa Tyson aliyejidhalilisha kwa kumng’ata sikio.
Uwezo wake ulimuwezesha kutwaa ubingwa wa uzito wa juu WBA, WBC na IBF.

USICHOKIJUA
Baadhi ya mambo usiyoyajua kwa mbabe huyo ambaye ni mdogo wa mwigizaji na mcheza muziki, Bernard Holyfield, Agosti 13, 2007 amewahi kujiingiza kwenye mchezo wa mieleka akicheza dhidi ya mbabe Matt Hardy lakini alijiondoa baada ya kuona mchezo huo haukuwa mzuri kwake.
Hali ya maisha anayoishi mbabe huyo yamemchachia kama ilivyo kwa Tyson kutokana na kukosa usimamizi wa mzuri wa fedha.
Mbabe huyo anelezwa kwamba amekuwa akiingiza kiasi kikubwa cha fedha kwa siku kilichofikia dola millioni 230.  
Matumizi mabaya ya fedha imekuwa sababu kubwa ya kufikia mbabe huyo kujikuta akiwa katika madeni hali iliyosababisha jumba lake la kifahari kuuzwa na benki mwaka 2008.
Mwaka jana amejikuta kwenye msukosuko mwingine wa kifedha akiwa anadaiwa fedha za kodi za mali zake hali iliyomfanya kuanza kuuza bidhaa zake za thamani.
Baadhi ya vitu alivyouza ni pamoja na medali ya Shaba aliyopewa kwenye mashindano ya Olympic, glovu zake jozi 20, ulingo, mikanda na kaptula zake 2
5 alizochezea mapambano.
JINAI
Tukio la kuuzwa kwa nyumba yake lilitokea Juni 2008 ambako alikuwa akishtakiwa na Benki ya Washington Mutual Bank waliotangaza jumba lake kuliuza ili kufidia deni lao la dola milioni 10.
Mjengo huo ulio kwenye eneo la ukubwa wa futi za mraba 54,000  jumla ya vyumba 109, vyumba vya kuoga 17 na lilitangazwa kuuzwa Julai 1, 2008 na baadaye liliuzwa kwa msanii Rick Ross kwa dola mil 17 kwa msanii Rick Rose.
Ama kweli mwaka wa matatizo ni matatizo kwani baada ya kumaliza hilo mwaka huo alijikuta matatani akishtakiwa na mzazi mwenzake, Toi Irvin kwa kosa la kutotoa fedha za matunzo ya mtoto wao kwa muda wa miezi miwili yaliyofikia dola 6,000.
Tatizo jingine likaibuka tena na kufikishwa mahakamani akidaiwa na Kampuni ya mazingira kiasi cha dola 550,000 kwa huduma waliyoitoa.
MAHUSIANO
Holyfield ni miongoni mwa wanaume waliobarikiwa kuwa na watoto wengi kwa bara la Amerika kwani ana watoto sita kwa wanawake tofauti.
Alinza kuwa na Toi Irvin ambaye ndoa yake ilivunjika na kuzaa naye mtoto mmoja na mapenzi yake akahamishia kwa Paulette Bowen aliyeachana naye akimuacha na watoto wanne.
Baada ya kutengana na mwanamama huyo Oktoba 4, 1996 alifunga ndoa na Dk. Janice Itson, ambaye wamefanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja na mwaka 2000 walitangaza kutengana.
Baada ya kutengana naye mwaka 2001 alioa mke mwingine Candi Smith, ambaye hawajafanikiwa kuzaa naye.
Fedha
Mbabe huyo ana utajiri unaofikia dola 500,000 (shilingi mil. 800)
Mwaka 199
2, Holyfield alipata dili la kutangaza biashara za kampuni za Coca Cola, Diet Coke, video game.
Makazi
Kwa sasa mbabe huyo anaishi eneo la Fayette County, Georgia ambako pia anafanya kazi ya kufundisha.

Wasifu
JINA: Evander Holyfield
UZITO: futi 6 inchi 2
URAI: Marekani
UMRI: 51
KUZALIWA: Atmore, Alabama

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...