Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 18, 2014

KAMERA PAMOJA NA WADAU KUFANYA ULINZI KATIKA NGUMI MARCH 29 PTA SABASABA


ALLY MWAZOA PROMOTA
WADAU wa mchezo wa masumbwi nchini Tanzania wamejitokeza kuwa walinzi wa mapambano yaliyo andaliwa na promota Ally Mwazoa yatakayoanza march 29, april 26 na mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba  akizungumzia mpambano wa Japhert Kaseba na Thomas mashali mpambano ambao umebakiza siku chache tu ili ufanyike

Mwazoa aliwashukulu wadau hawo ambao wamejitokeza kwa ajili ya ulinzi wa ali ya juu utakaofanyika siku hiyo kwa mabondia na wadau wenyewe kukubali kulipa kiingilio na kufanya ulinzi wa kila kona katika ukumbi huo 
ambapo klabu mbalimbali za ngumi kutoka Temeke Ilala Kinondoni na Tanga pamoja na mikoa ya jirani na wadau wamejitokeza kuthibiti fujo mbalimbali ambazo zitajitokeza siku hiyo pia wale ambao wamedhamilia kufanya fujo siku hiyo kutakuwa na askari kanzu mbalimbali hivyo watapata kipondo cha ali ya juu pamoja na kutupwa lupango

Mwazoa aliongeza kwa kusema siku hiyo kutakuwa na kamera maalumu zitakazofungwa kila upande wa ukumbi huo ili kuona matukio mbalimbali ya nje na ndani yatakayokuwa yakiendelea ili kuthibiti vitendo vya uhuzwaji wa tiketi feki na kuingia kiolela na kusababisha asara kwa promota na washiliki katika tukio zima

aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi makali ambapo bondia Haji Juma atavaana na Juma Fundi wakati Fred Sayuni atapambana na Rajabu Mahoja na Zuber Kitandula atamenyana na Issa Omar wakati Bakari Dunda ataoneshana ubabe na Baina Mazola

       Mwazoa

aliongeza kuwa ulizi na usalama wa mali zako ni wa huwakika hivyo familia nzima mnaweza kuja kushudia mpambano huo wa masumbwi bila shaka 
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...