Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 14, 2014

RAIS KIKWETE AWAAPISHA KATIBU NA NAIBU KATIBU WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA


 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Katibu na naibu katibu wa Bunge Maalum la katiba katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Dodoma leo.  Waliokula kiapo mbele ya Rais ni Katibu Bwana Yahya Khamis Hamad na naibu wake Dkt. Thomas Kashililah. 

Katibu Wa Bunge Maalum la Katiba Bwana Yahya Khamis Hamad (pichani juu) na Naibu wake Dkt.Thomas Kashililah (Pichani chini) wakila kiapo mbela ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla iliyofanyika Ikulu ndogo mjini Dodoma leo. Wapili (kushoto) akishuhudia kiapo ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu.
Picha na Freddy Maro.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Samwel Sitta (kushoto) akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo Pandu Ameir Kificho wakati wa Hafla ya kuwaapisha Katibu na Makamu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.Katikati ni Mjumbe wa Bunge hilo na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Mwenye tai ya bluu) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta (kulia), Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. na Naibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila (Kushoto kwa  Katibu wa Bunge) Leo Mjini Dodoma.
Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Yahya Khamis Hamad akipokea vitabu vya muongozo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.
Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw, Thomas Kashilila akipokea vitabu ya muongozo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwaeleza jambo Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kulia kwa Rais) akifuatiwa na  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta, Prof. Mark Mwandosya na Mwisho Pindi Chana.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimweleza jambo Naibu Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Juma Nkamia wakati wa Hafla ya Kuapishwa kwa Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Leo Mjini Dodoma. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...