Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 13, 2014

KUMBE WASTARA KAZAA NA SOLO THANGStori: Joseph Shaluwa
IMEBUMBURUKA! Kumbe staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma, aliye mama wa watoto watatu, mmoja kati yao, alizaa na mkongwe katika Bongo Hip Hop, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’.
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika kilipasha kuwa Wastara amekaa na siri hiyo moyoni kwa muda mrefu sana.
Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma.
“Mtoto mmoja alizaa na Solo, wakati ule Solo akiwa anatamba na nyimbo zake kama Homa ya Dunia, Mambo ya Pwani na Mtazamo ambao alishirikiana na Afande Sele na Profesa Jay. Tena leo (juzi Jumatano) ameandika kwenye Instagram na ameweka na picha ya Solo,” alipasha shosti huyo.
Msafiri Kondo a.k.a Solo Thang.
Haraka paparazi wetu, akazama kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kufanikiwa kuona picha hiyo iliyosindikizwa na maneno: “Baba wa baby wa miye, Msafiri Kondo a.k.a Solo Thang, moyo wako haukupishana sana na wa Sajuki (Juma Kilowoko).
“Sijawahi kuyasema haya lakini utazipata salamu huko ulipo. Maisha yametutenganisha ila sijawahi kugombana na wewe wala familia yako. Nashukuru kwa upendo wenu juu yangu hasa mama yako. Nawapenda sana na hata mtoto wenu anawapenda. Dunia ni njia tu, hatujui nani atatangulia. Nakutakia mafanikio. Inshallah.”
Risasi Jumamosi lilimpandia hewani Wastara ili kupata ufafanuzi juu ya ishu hiyo ambapo alikuja juu: “Hivi kwa nini mnanifuatafuata sana jamani? Sasa umesema umeona Instagram, kwa hiyo nikusaidie nini?”
RISASI JUMAMOSI:
Nataka kujua machache kuhusu Solo na huyo mwanaye. Mlianza lini uhusiano na kwa nini ulikaa kimya kwa muda mrefu. Ni muhimu ufafanue hili Wastara, maana umeweka kwenye mtandao wa kijamii na wengi wameona.
WASTARA:
Naomba mniache, nina mambo mengi yananisumbua kichwani mwangu. Kama wameona, acha waone. (Tiiii...tiii...tiiii.... Wastara alikata simu).Chanzo:www.globalpublishers.info

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...