Kocha mpya wa timu ya African Lyon inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Pablo Ignacio
Velez kutoka Argentina wa kwanza kulia,
akizungumzia nini atafanya akiwa na timu
hiyo kwa ajili ya msimu ujao uliopangwa kuanza Septemba Mosi mwaka huu. Kocha
huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo. Wengine katika picha ni
Charles Otieno ambaye ni mkurugenzi wa ufundi na Biashara wa timu hiyo na
Meneja Mkuu na Mmiliki wa timu hiyo, Rahim Kangezi. Picha na Mpiga picha wetu.
Mwandishi wetu
KOCHA mpya wa timu ya soka ya African Lyon, Pablo Ignacio Velez, amewasili nchini tayari kuanza kuinoa timu hiyo na kuomba apewe muda wa kukisuka upya kikosi hicho huku akiahidi mabadiliko zaidi ya soka kwenye timu hiyo.
Pablo raia wa Argentina aliyasema hayo jana baada
ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo na kusisitiza
lengo lake kubwa ni kuhakikisha vijana wanapewa nafasi ya kuonyesha
vipaji vyao na ndivyo itakavyokuwa Afrika Lyon.
"Sikuja
Tanzania kutafuta pesa, ndoto yangu kubwa ilikuwa kufundisha soka barani
Afrika hivyo wakati ni sasa," alisisitiza kocha anayezungumza lugha ya
'kiispanyola'.
Pablo alisema "kazi ya aina yoyote lazima ipewe
muda na mchezaji lazima atengenezwe hivyo watanzania wawe na subira kwa
ajili ya kupata matunda mazuri ya vijana hapo baadae kutoka African
Lyon.
Kocha huyo aliyewai kuzichezea timu za taifa za vijana
chini ya miaka 17 na 20 za Argentina hakusita kusisitiza suala la
nidhamu kwa wachezaji wa timu hiyo ya ndani na nje ya uwanja.
"Nidhamu
ni muhimu kwa wachezaji wangu cha msingi tushirikiane katika
kufanikisha hili kwa vijana kwani mchezaji anatakiwa kati ya miaka 18 na
19 awe ametengeneza jina kupitia soka ," alisema Pablo.
Naye Mmiliki wa African Lyon, Rahmu Kangezi alisema lengo la kumleta kocha huyo ni kuhakikisha timu hiyo inajongea mbele zaidi.
Kangezi
alisema licha ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja lakini wanaweza
kumtumia Pablo kwa kipindi kirefu kulingana na mfumo wa kuhakikisha
wanaendeleza vijana katika timu yao.
"Pablo ni zaidi ya kocha,
ana uwezo pia amecheza mpira pia ni kocha wa kwanza kutoka Argentina
kuja Tanzania hivyo tunaimani timu yetu ya African Lyon itafika mbali
zaidi kisoka," alisitiza Kangezi.
Pablo mwenye miaka 38 aliyechukua mikoba iliyoachwa na Jumanne Chale amewai kuifundisha klabu ya Atletico Colo Colo De Chile (1998).
Pablo mwenye miaka 38 aliyechukua mikoba iliyoachwa na Jumanne Chale amewai kuifundisha klabu ya Atletico Colo Colo De Chile (1998).
Klabu
nyingine alizowai kufundisha ni Atletico Calchin (2000), Atletico
Belgrano De Cordoba (1997), Atletico River Plate (1993-1995).
Klabu
nyingine ni Banco De Cordoba (1991 na 1997), Deportivo Lasallano (1992)
Atletico Argentino Penarol kwa miaka minne na klabu nyingine nyingi za
Hispania na Argentina
NASHUKURU ATA KWENYE PICHA YAKO YA TIMU YA TAIFA YA NGUMI KUNA ZAO LA KEKO ,KARIBU
ReplyDeleteNIMEONA CHALINZE LAKINI NI MUHIMU KUJIPANGA AU KUSHIRIKISHA WADAU WENGINE KUHAKIKISHA KILA KITU KINAKWENDA SAWA ,UWANJA HASWA SEHEMU YA SAKAFU PENGINE UKIUNGANA NA WADAU WENGINE UNAWEZA KUPATA KITU BORA ZAIDI .
ReplyDeleteHONGERA KAKA