Wasanii hao wakionyesha baadhi ya Kazi zao faki ambazo wamezikamata eneo la Kariakoo hivi karibuni. |
Msanii wa Filamu Nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto akizungumza na waandishi wa habari wakati walipokuwa wanatoa tamko lao kwa waandishi hao kuwa wameungana kupambana na maharamia wa kazi zao za sanaa kushoto ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na msanii Muhsin Hawadh.Picha na www.burudan.blogsports.com. |
SHIRIKISHO
la Filamu nchini(TAFF) kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za usambazaji wa
filamu na kazi za wasanii ‘zimeapa’ kupambana na maharamia wote wa kazi hizo
ili kulinda maslahi ya wasanii.
Wakizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo, umoja huo kwa pamoja ulisema
umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili
kuzima mianya yote ambayo ni kero kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho hilo Simon
Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake
ya kuwasaidia wasanii kwa kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila
pembe ya nchi hii huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.
“Umefika wakati kwa Serikali kusikia
kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya
wasanii wanaoendelea kuwa masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu
wachache wanaoiba kazi zao”
“Tuna imani kuwa kama kazi za
wasanii zitasimamiwa vizuri, tutaweza kuongeza pato la Taifa kwa kiwango
kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio
isipokuwa kuna watu wachache ndiyo wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba.
Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii.
Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii.
Alisema Serikali inapswa kuonyesha
makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza
nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.
Kwa upande wake Meneja usimamizi
kutoka TRA Msafiri Ndimbo alisema Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa
kazi hizo kuanzia Januari Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake
kukubalina kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo. Ambapo wasanii na
wasambazaji wa kazi zao wameungana pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao
zinakwebnda kwa haki ili wasanii wapate na wao wawe ni watu wa kusaidi wasanii
kusambaza kazi zao.
No comments:
Post a Comment