Toka
kushoto, Kocha Remmy Ngabo(ngumi), Kanali Pellegreen Mrope (Afisa
Ulinzi, Ubalozini), Kocha Zachariah Gwandu (riadha) na Amos
Msanjila(Afisa Mambo ya Nje Ubalozini, Daraja la Pili ).
Mwanahabari
Frank Eyembe wa Urban Pulse (katikati) akiwa na kocha wa kuogelea,
Sheha Mohammed Ali na kocha wa masumbwi, Remmy Ngabo katika tafrija
ndogo kuwaaga wanamichezo wetu London.
Balozi
wetu Peter Kallaghe akiwa na wahudumu wa Olimpiki wasiolipwa mshahara,
Lesley Shayler, Alison Cochrane na Steve Wiseall. Wa kwanza kulia ni
Balozi wa Rwanda, Uingereza Mheshimiwa Ernest Rwamucyo.
Balozi
wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe( wa nne aliyesimama
nyuma toka kulia) akiwa na wanamichezo, makocha, maofisa na wahudumu wa
kujitolea Olimpiki. Kulia kwake ni mkuu wa msafara, Bwana Hassan Jarufu
na Balozi wa Rwanda, Mheshimiwa Ernest Rwamucyo (wa kwanza kulia)
nyumbani kwake alipowaalika kuwapongeza na kuwaaga jana Jumatatu.Picha
Zote na Freddy Macha
--
Balozi
wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe amewapongeza
wanamichezo wetu walioiwakilisha nchi katika Olimpiki kwa nidhamu na
kuwataka wasivunjike moyo kwani sio sisi tu tuliokosa medali.
“Wanamichezo
wetu wameonyesha tabia bora kinyume na watu wa nchi nyingine waliofanya
mambo ya aibu sana. Lazima tuwapongeze kwa kufikia viwango na kuibeba
bendera ya Tanzania,”alisema.
Akiongea
katika tafrija ndogo kuwaaga wanamichezo saba, maofisa na makocha wao,
Balozi Kallaghe alisisitiza kwamba tusiwalaumu wanamichezo kwa
kushindwa kwani kuna mataifa mengi yaliyokosa medali. Tafrija hiyo
ilihudhuhuriwa na maofisa wote wa Ubalozi, wanahabari London na Balozi
wa Rwanda Uingereza, mheshimiwa Ernest Rwamucyo.
Kitakwimu ni asili mia kumi tu ya washiriki 10,500 waliocheza michezo 26 (toka mataifa 204) wakapata medali.
“Kuna
mataifa tajiri kama Ujerumani, Australia na India ambayo hayakufanya
vizuri na pia wenzetu Afrika mfano Kenya na Ethiopia ambao hawakuridhika
au kufikia nafasi waliyozoea miaka iliyopita.”
Balozi
aliitaja nchi ya Wafilipino (Philippines) yenye watu Millioni 93 ambayo
ilikuwa na wachezaji 11 na haikuambulia kitu. Kidesturi toka 1936,
Wafilipino wamekuwa wakishinda medali katika mchezo wa ngumi.
“Lazima
tujiulize maswali ili kufanikiwa mashindano yajayo na kujitayarisha
ndiyo msingi. Vipaji vingi vipo Tanzania. Tujaribu kuangalia na
kujiuliza wapi vilipo vianzio vya kuendeleza michezo yetu kutoka ngazi
za chini maana uwezo wa kushinda tunao. ”
Akipigiwa
makofi balozi alimtaja mkimbiaji maarufu wa Uingereza mwenye asili ya
Kisomali, Mohammed “Mo” Farah aliyefanya vibaya sana Olimpiki ya 2008,
China. “Baada ya kushindwa kabisa Beijing, Mo Farah alijilaumu na kulia
sana; ila hakuvunjika moyo; alirudi akajiandaa vizuri na matokeo yake
mwaka huu kashinda medali mbili za dhahabu.”
Naye
mkuu wa msafara Bwana Hassan Jarufu aliushukuru ubalozi wetu Uingereza
kwa ukaribisho mzuri uliohakikisha kwamba wanamichezo wako sawa toka
walipowasili hapa majuma mawili kabla ya Olimpiki. Aliwataja pia
wasaidizi wenyeji wa Uingereza, Alison Cochrane, Steve Wiseall na Lesley
Shayler aliyewahi kuitembelea Bongo na kuipenda sana.
“Hawa wamekuwa wenyeji wetu wazuri sana,” alisema.
Bwana
Jarufu alifahamisha kwamba wanamichezo wetu shurti kupongezwa kwa
kujitahidi kufanya shughuli hii bila ajira au kazi maalum.
“Kwa
mfano wakimbiaji wa mbio za marathon wanatakiwa kiafya wakimbie mara
nne tu kwa mwaka kusudi wawe tayari kwa mashindano makubwa, lakini
kutokana na kukosa ajira au msaada wa kifedha wanalazimika kushindana
mara nyingi zaidi ili waishi. Na si ajabu ukamsikia mmoja mmoja
akilalamika kashindwa mashindano makubwa kama Olimpiki kutokana na
majeruhi fulani mwilini.”
Katika
michuano ya siku ya mwisho Jumapili wanariadha watatu, Faustin Mussa,
Samson Ramadhan na Mohammed Msondiki Ikoki walishiriki mbio za marathon
na hawakupata medali yeyote. Mshindi alitoka Uganda Stephen Kiprotich
akifuatiwa na Wakenya: Abel Kirui na Wilson Kiprotich.
Habari zaidi tembelea :www.kitoto.wordpress.com
No comments:
Post a Comment