MWIMBAJI wa muziki wa Taarab Mwanne Othman Sekuru pichani juu ambaye anatamba katika wimbo wa Vifuu Tundu alioshirikishwa na AT,ambao pia ulipenya na katika tuzo
za muziki za Kilimanjaro 2012 sasa kuipua kibao kingine baada ya
sikukuu ya Idd El Fitr wimbo huo unakwenda kwa jina la ‘Midume
Mashauzi.
Akizungumza leo Mwanne alisema kwamba mashabiki wake wakae mkao wa kupata raha kwani katika wimbo huo ameachia madongo ambayo kama mtu atakuwa na tabia hizo basi dongo hilo litakuwa ni sawasawa kwa muhusika.
"Katika
wimbo huo ambao tumeimba pamoja umetungwa na Mohammed Omari Mkwinda
‘Meddy’ ambaye mara baada ya kuutunga akaniletea namimi nikaweka maneno
ya kutia nakshi kama, Watashindana lakini watashindwa wenyewe na mengine
mengi kama ‘hunathamani kama mkia wa mbuzi hufuniki wala hufukuzi nzi’
na mengine mengi tu".
Mwanne ambaye mbali ya kuwa muimbaji
katika kundi la Jahazi Modern Taarab pia ni mtangazaji wa kipindi cha
‘Tamtam za Mwambao’ kinachorushwa katika kituo cha redio ya East Africa
‘EATV’.
No comments:
Post a Comment