Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Exim Bw. Anthony Grant akikata utepe kuashiria
makabidhiano ya madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni nane kwa
Shule ya Msingi ya Kilakala iliyopo katika Manispaa ya Temeke jijini Dar
es Salaam jana. Kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Abdul
Kutarasa, Diwani wa Kata ya Kilakala, Elizabeth Magwaja (wapili kulia)
na Afisa Elimu Manispaa ya Temeke, Angela Frank (wapili kushoto). Picha
na Mpiga Picha wetu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Exim Bw. Anthony Grant akiteta jambo na mmoja wa
wanafunzi wa shule msingi Kilakala wakati wa hafla fupi ya makabidhiano
ya madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni nane kwa Shule ya
Msingi ya Kilakala iliyopo katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es
Salaam jana. Akishuhudia watatu kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa Benki
y Exim N. Seshagiri Rao. Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Exim Bw. Anthony Grant akisalimiana na mmoja
wanafunzi wa shule msingi Kilakala muda mfupi kabla ya kukabidhi
madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni nane kwa shule hiyo
iliyopo katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu
BENKI
ya Exim Tanzania imetoa mchango wa madawati 100 yenye thamani ya
shillingi milioni nane kwa shule ya Msingi ya Kilakala iliyopo Manispaa
ya Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mchango wa benki hiyo
kwa jamii.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi madawati hayo jijini Dar es Salalam leo,
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Anthony Grant benki inayosherehekea
miaka 15 tangu ianzishe mwezi huu wa Agosti alisema benki inaelewa
umhimu wa elimu katika maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Grant
alitangaza kuwa benki yake itakuwa mlezi wa shule hiyo huku ikisema
kuwa benki yake itakuwa mstari wa mbele kukabiliana na matatizo
mbalimbali yaliyopo shuleni hapo.
Grant
alisema kuwa pamoja na kutoa madawati 100, benki yake itaendelea
kuisadia shule hiyo katika maeneo mbali mbali baada ya kufanya uchunguzi
uliothibitisha kuwa shule inakumbana na changamoto mbalimbali ikiwa ni
pamoja na ukosefu wa madawati.
“Leo
hii tunatangaza mahusiano mapya baina ya Benki ya Exim na Shule ya
Msingi ya Kilakala. Leo hii tunakabidhi madawati 100 lakini pia tutaendelea kuisadia shule katika maeneo mengine kwa awamu.
“Tunaimani
kuwa mahusiano yetu yatahakikisha kuwa shule inakuwa katika mazingira
mazuri ya kujifunzia. Tunatambua umuhimu wa elimu katika nyanja zote
mbili za kijamii na kiuchumi na ndiyo maana tumeamua kutoa mchango wetu
katika masuala mbalimbali ya kielimu,” alisema.
Bw.
Grant alisema kuwa benki yake imeona umuhimu wa kujikita zaidi kwenye
shughuli chache za kijamii ambazo zitaleta mabadiliko chanya badala ya
kuelekeza misaada michache ya kifedha katika shughuli mbalimbali za
kijamii.
“Tukisharidhika
kuwa tumeshafikia lengo letu na shule imeshapata kila kitu muhimu,
baada ya hapo tutaendelea na mradi mwingine kwa kutumia falsafa ileile,”
alisema.
Kwa
upande wake Mkuu wa Shule hiyo ya msingi Abdul Kuratasa aliepokea
madawati hayo kwa niaba ya shule aliishukuru benki kwa msaada wake
uliowafikia katika wakati muafaka na kuhaidi kuyatunza na kuyatumia
madawati hayo vizuri.
“Tunafuraaha
sana kuwa Benki ya Exim imeridhia maombi yetu. Tunaimani mahusiano yetu
haya mapya yatatuwezesha kujenga mazingira mazuri ya kujifunzia,”
alisema.
No comments:
Post a Comment