Rais wa Chama Cha walimu Tanzania Bw. Gratian Mukoba (Kushoto)
akiongea na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Chama hicho jijini
Dar es Salaam kuhusiana na Tamko lao kwa
serikali kutaka iwarudishie madaraka wakuu wote waliovuliwa nyadhifa zao
kwakuwa ni viongozi wa (CWT) ndio waliohamasisha mgomo.
Vilevile chama hicho kimeitaka
serikali kufuta nia yake ya kuwashitaki
walimu zaidi ya 180,000 walioshiriki mgomo kati ya walimu 233,440 walioko
nchini kwani kwa kufanya hivyo watoto wa maskini wanaotegemea walimu hao
kufundisha watakosa haki yao ya kufundishwa.Kulia na Kaimu katibu mkuu wa chama hicho Bw, Ezekiel Olotu.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
)Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano
huo wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Chama cha walimu CWT nchini.
No comments:
Post a Comment