Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akizungumza
katika mkutano huo. Kulia kwake ni Ofisa Tarafa wa Magomeni, Flugence
Isakefu, Mhariri Mtendaji wa Global, Richard Manyota na Mratibu wa
shughuli mbalimbali za Glabal, Juma Mbizo.
Abdallah Mrisho akionyesha mojawapo ya simu aina ya Samsung Galaxy ambazo zitashindaniwa sambamba na Noah hiyo.
Gari aina ya Noah linaloshindaniwa.
Picha ya pamoja ya baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo.
KAMPUNI ya Global Publishers ambayo huchapisha magazeti ya Ijumaa
Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, leo imezindua rasmi
shindano la ‘Shinda Noah’ katika ofisi zake zilizopo Bamaga, Mwenge,
jijini Dar.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo wa uzinduzi, Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho, amesema huo ni utaratibu ambao kampuni imejiwekea kurudisha sehemu ya mapato kwa wateja wake na kama ilivyokuwa kwa miaka mitano iliyopita, mwaka huu gari aina ya Noah litatolewa.
“Mbali na zawadi hiyo ya gari, zawadi nyingine ambazo ni simu za mkononi, televisheni, na nyingine kibao zitatolewa kwa wasomaji wa magazeti pendwa na kwa kutuma kuponi kwa anuani elekezi,” alisema Mrisho.
Mgeni rasmi katika promosheni hiyo inayoanza mwezi huu wa Agosti na ambayo itafikia kikomo mwezi Novemba, alikuwa ni Ofisa Tarafa wa Magomeni, Flugence Isakefu, ambaye alifika kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Lugimbana.
PICHA/PICHA : ERICK EVARIST NA RICHARD BUKOS / GPL

No comments:
Post a Comment