Wachezaji wa Taifa stars wakiwasili Gaborone
Kikosi
cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kikiwa na wachezaji 17
kimewasili leo asubuhi jijini Gaborone tayari kwa mechi ya kirafiki ya
kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya
wenyeji Botswana 'Zebras' itakayochezwa kesho (Agosti 15 mwaka huu).
Stars imetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama saa 5.45 leo asubuhi kwa saa za hapa
ambapo nyumbani ni 6.45 na kupokewa na viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Botswana (BFA) na
Watanzania wanaoishi hapa Botswana.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Boniface Wambura baadhi ya wachezaji walioko kwenye
kikosi hicho ni Frank Domayo, Ramadhan Singano na Simon Msuva
ambao walijiunga na Stars saa chache baada ya kurejea kutoka Nigeria ambapo walikuwa na timu ya vijana
wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) ambayo Jumapili ilicheza mechi ya mashindano ya Afrika
dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).
Wachezaji wengine kwenye kikosi kilichoko Botswana ni Aggrey Morris, Amir Maftah, Athuman Idd, Erasto
Nyoni, Haruna Moshi, Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa, Mwadini Ally, Mwinyi Kazimoto,
Ramadhan Chombo, Salum Abubakar, Said Bahanuzi na Shabani Nditi.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia kwenye hoteli ya Oasis ambayo pia ndipo
Zebras imepiga kambi kwa ajili ya mechi hiyo. Mechi itaanza kesho saa 1 kamili usiku kwa saa za hapa na
itafanyika kwenye Uwanja wa Molepolole Sports Complex. Uwanja wa Taifa wa Botswana hivi sasa uko
kwenye matengenezo.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema mechi hiyo ni muhimu kwa vile timu yake bado
inakabiliwa na mechi za Kombe la Dunia Kanda ya Afrika, na michuano ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji
wa Ndani (CHAN) inayotarajia kuanza baadaye mwaka huu.
TAIFA STARS YAKWEA PIPA TAYARI KWA MECHI YAO NA BOTSWANA
Nahodha
wa timu ya Taifa, Taifa Stars Juma Kasseja akiwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya safari ya
kwenda Gaborone, Botswana kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho
Jumatano .
Wachezaji
wa timu ya taifa, 'Taifa Stars' Mrisho Ngassa na Haruna Moshi 'Boban'
wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya safari ya kwenda Gaborone, Botswana kucheza
mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho Jumatano.
Wachezaji
wa timu ya Taifa,Taifa Stars wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya safari ya
kwenda Gaborone, Botswana kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho
Jumatano.
No comments:
Post a Comment