Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 9, 2013

Adolf Mbinga aanza mambo Sikinde Ngoma ya Ukae


Adolf Mbinga akiwa kazini


NA MWANDISHI WETU
WASHABIKI wa muziki waliohudhuria onyesho la Jumapili la bendi hiyo lililofanyika kwenye ukumbi wa Sigara Chang'ombe jijini Dar es Salaam walianza kushuhudia kazi ya kwanza ya mpiga solo mpya wa bendi ya Mlimani Park Adolf Mbinga.
                          
Mbinga aliyejiunga na bendi hiyo akitokea bendi mbalimbali zikiwemo African Stars 'Twanga Pepeta' Mchinga Sound na nyingine kadhaa alianza kuonyesha uwezo wake katika wimbo wa kwanza aliopiga na bendi hiyo unaoitwa 'Kukatika kwa Kidole Gumba'
Katika wimbo huo uliotungwa na Hassan Reheni Bitchuka, Mbinga alionyesha uwezo mkubwa katika ukung'utaji wa gitaa la solo.
Akizungumza katika onyesho hilo, Mbinga alieleza kuridhishwa kwake kuwepo kwenye bendi hiyo yenye wanamuziiki wenye uwezo na vilevile wanaojua jinsi ya kuishi na wenzao.
Alisema anakusudia kushiriki zaidi mkakati wa kuirudisha bendi hiyo kwa wapenzi wake katika siku chache zijazo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...