Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 9, 2013

WADAU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MWANZA (MPC) WAJITOKEZA KUCHANGIA UNUNUZI WA MASHINE YA KUCHAPISHA MAJARIDAMwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Mwanza (MPC) Deus Bugailwa akitamka ahadi za watu mbalimbali na mashirika ambayo hayakufanikiwa kufika katika Harambee hatua ya Mwanza ya kuchangisha fedha ili kununua mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti mbele yake ni Rais wa UTPC Keneth Simbaya. Harambee hiyo ilifanyika katika ukumbi wa JB Belmont Mwanza.

Meneja wa Kanda wa Benki ya NMB Straton Chilongola (wa pili kulia) akiwa na Meneja Mawasiliano wa benki hiyo Bi. Josephine Kulwa wakikabidhi hundi ya shilingi milioni mbili kwa Rais wa UTPC Keneth Mbaya, katika kuchangia harambee ya ununuzi wa mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti. Kushoto kabisa ni Mwenyekiti wa MPC Deus Bugailwa.  

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani Mhe. Stanslaus Mabula alitoa kauli ya ofisi yake kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja kwenye harambee ya ununuzi wa mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti, iliyofanyika Hotel JB Belmount Mwanza.

Ni mkono wa shukurani kutoka kwa mwenyekiti wa MPC Bw. Deus Bugahilwa kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula. Hata hivyo meya huyo hakukaa sana kwenye harambee hiyo kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine ya kijamii, hivyo aliomba radhi na kuondoka. 

Ilikuwa ni zamu ya Brother kutoka Mwananchi Communication Fredrick Katulanda.

Na hapa ilikuwa ni zamu ya mdau kutoka New Habari Cooperation Grace Chilongola.

Brother Jimmy Luhende hakulichukulia suala hili mzaa alikuja na mpunga wa kutosha wa kitu 'cash'.

Mwanasheria wa Kampuni ya vyombo vya usafiri majini Marine service hakuwaangusha wanahabari.

Naye katibu wa MPC alihusika changizoni.

Meza ya Mwandishi wa habari wa ITV Mwanza Mabere Makubi ilipendeza sana.

CEO wa Gsengo blog Mr. Albert G. Sengo akiwasilisha mchango wake katika harambee ya kuchangisha fedha ili kununua mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...