Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 22, 2013

FLAVIANA MATATA ASHIRIKI MISA YA KUMBUKUMBU YA AJALI YA MV BUKOBA


 Flaviana Matata akiwasha mshumaa katika kaburi la Mama yake mzazi aliyefariki dunia katika ajali ya Meli ya Mv Bukoba, ikiwa ni miaka 17 tangu ilipotokea ajali hiyo ilipotokea. Flaviana aliwasha mshumaa huo ikiwa ni ishara ya kuomboleza akiungana na ndugu jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo, ambapo shughuli hiyo imefanyika leo katika Makaburi ya Igoma, jijini Mwanza, walikozikwa baadhi ya marehemu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
 Flaviana Matata akishirikiana na ndugu, jamaa na marafiki na baadhi ya waombolezaji waliopoteza ndugu zao katika ajali ya Meli ya MV Bukoba, wakiwasha mishumaa kwa pamoja ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka, wakati wa Ibada maalum ya kumbukumbu ya ajali hiyo.
 Flaviana Matata akiwa na Baba yake mzazi na ndugu, jamaa na marafiki katika Misa ya  maombelezo  Ajali ya MV Bukoba. Misa hiyo imefanyika leo, Igoma Jijini Mwanza.
Flaviana Matata akiwasili ofisini kwa Projest  Samson Kaija, ambaye ni General Manager wa Marine Services Company Ltd, ambao hushirikiana naye katika maombolezo ya Ajali hiyo ambapo mwaka jana aliwapa msaada wa maboya ya kuokolea maisha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...