Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 24, 2013

Afande Sele kuachia albamu ya ‘Amani na Upendo’


Na Elizabeth John

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye anauwakilisha mkoa wa Morogoro, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ ameachia albamu yake mpya inayojulikana kwa jina la ‘Amani na Upendo’.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, alisema licha ya soko la mauzo ya albamu kusuasua hatojali mauzo mabaya kwakuwa lengo lake ni kuelimisha jamii na sio kupata maslahi.

“Sitofikilia soko kama litalipa au vipi ninachohitaji ni kuwapa elimu watanzania, mashabiki wategemee kununua albamu hiyo kwa bei rahisi,” alisema.

Alisema anaomba mashabiki waipokee vizuri kazi hiyo na kwamba ina jumla ya nyimbo 10 ambazo zote zimefanya vizuri katika soko hilo.

Afande sele alizitaja baadhi ya nyimbo ambazo zipo katika albamu hiyo kuwa ni Kingdom, Karibu Morogoro, Karata Dume na nyinginezo ambazo zinafanya vizuri katika soko hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...