Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 30, 2013

KASEBA APANIA KUMKALISHA MMALAWI


Na Elizabeth John


BONDIA wa ngumi za mateke ‘Kick Boxer’ Japhet Kaseba amesema amejipanga kuweka rekodi nzuri katika tasnia hiyo kwa kumchapa Mmalawi, Rasco Chimwanza katika pambano lao la kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati linalotarajiwa kuchezwa Juni 8, mwaka huu.Akizngumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema anajua kama bondia huyo ni nyota katika tasnia hiyo, lakini kutokana na maandalizi aliyoyapata atahakikisha anaweka heshima katika ngumi za mateke.
“Namshukuru mungu nina afya nzuri hadi sasa na naendelea na mazoezi kwajili ya pambano hilo naomba Watanzania wajitokeze kwa wingi katika ukumbi huo wa DDC Magomeni,” alisema Kaseba.
Naye Katibu Mkuu wa Oganizasheni ya ngumi ya za kulipwa Tanzania (TPBO), Ibrahim Kamwe alisema maandalizi ya pambano hilo yamekamilika, na tayari wamemtumia nauli Mmalawi huyo na kwamba anategemea kuingia nchini Juni 5.
Alisema TPBO imemtengenezea mazingira mazuri ya ushindani, Kaseba na kwamba wanategemea atafanya vizuri katika pambano hilo kutokana na maandalizi ambayo anaendelea kufanya.

 Nae kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia  wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
 
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila ,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe. 
 
 mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...