Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 9, 2013

MISS EARTH TANZANIA 2012, BAHATI CHANDO KUANDAA HAFLA YA MOTHER'S DAY mei 12 JIJINI DARPichani kati ni Miss Earth Tanzania 2012,Bahati Chando akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo kwenye hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day", siku ya Mama Duniani  itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo, ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu imepangwa kuwa ni "always in our heart's", "tukiwakumbusha akina  mama zetu kwamba wapo moyoni mwetu na tunawapenda sana" alisema Chando. 

Shoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa na kulia ni Mratibu wa hafla hiyo, Bi.Regina Ogwalla. Bahati amesema kuwa katika hafla hiyo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mwenyekiti wa UWT Ilala,Mh.Nora Mzeru.

Miss Earth Tanzania 2012,Bahati Chando amesema kuwa ameamua kuungana na Diwani wa kata ya Kipawa, Mh. Bonnah Kaluwa kuandaa hafla hiyo itakayozinduliwa na Wamama wa Ilala,kutambua umuhimu wa kina mama,kuwafurahisha lakini pia kuwaelimisha kuhusu mambo mbalimbali,amesema kuwa amekuwa na shauku kubwa ya kuandaa sherehe kama hiyo ili kujitoa na kusaidia watu kama watu wengi walivyoungana kumsaidia katika safari yake ya kuwa  mrembo wa kupeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa.

Pia anasema kuwa ameandaa sherehe hiyo kuonyesha jamii kwamba,kuwa mrembo au miss sio tu kupozi mbele ya Kamera,bali inaambatana na na jukumu la kugusa jamii kwa namna mbalimbali.
Shoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa akitoa ufafanuzi  kuhusiana na  uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day",siku ya Mama Duniani  itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo,ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu kwenye hafla hiyo umepangwa kuwa ni "always in our heart's",

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...