Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 22, 2013

SUMA MNAZARETI AHOJI 'TUPO WANGAPI'


Na Elizabeth John

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Suma Mnazareti amesema
anatarajia kuachia kibao chake kipya hivi karibuni kinachokwenda
kwa jina la ‘Tupo wangapi’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,Suma alisema katika kibao hicho
ameshirikiana na msanii nyota wa muziki huo kutoka katika kundi
la Tip Top Conection yenye maskani yake Manzese Dar es Salaam,
Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’.
“Unajua kila msanii ana mashabiki wake hivyo naamini kutokana
na kufanya kazi na msanii huyo ninaimani kibao changu
kitapokelewa vizuri na mashabiki wa tasnia ya muziki huo,”.
alisema Suma Mnazaleti.
“Nashukuru kazi zangu zinapokelewa vizuri na mashabiki kitu
ambacho kinaniongeza uwezo wa kuendelea kuandaa kazi nyingi
ili kuendelea kufurahisha jamii pamoja na kuelimisha kupitia fani
hii,” alisema.
Alisema amekuwa akiumiza kichwa kila siku kwa ajili ya
kutengeneza vitu vizuri vyenye ujumbe kwa jamii lengo lake likiwa

ni kutoka kimaisha kupitia muziki.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...