Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 27, 2013

GARI LAGONGA TRENI DAR MKE ALIYEKUWA AKINDESHA YUPO TAABANI MUME WAKE AFA PAPO HAPO


Wakazi wa Dar es Salaam wakingalia eneo ajali hiyo ilipotokea majira ya asubuhi leo.
 
Treni likiendelea na huduma zake likipita jirani na eneo lilipogongana na gari dogo aina Honda CRV jirani na Moshi Bar Dar es Salaam asubuhi leo. Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni mume wa dereva wa gari hilo alifariki papo kwa hapo. Mwanafunzi wa shule aliyejulikana kwa jina la Grace Samsoni alipata michubuko  wakati wa ajali hiyo alitibiwa na kuruhusiwa katika hospitali ya Amana.
 
Baadhi ya wakazi wa eneo la Moshi Bar karibu na Mombasa nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakiangalia kioo cha gari aina ya Honda CRV eneo ajali ilipotokea. 

Agnes Msoka aliyekuwa akiendesha gari lililogonga treni na kusababisha kifo akisubiri kufanyiwa upasuaji hospitalini.
 
Dereva wa gari liligonga Treni akiwa amelazwa ICU kwa matibabu.

Gari iliyogonga treni likiwa limeegeshwa Kituo cha Polisi Kikuu cha TAZARA Dar es Salaam.

Huyo ndo marehemu aliyefariki katika ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...