Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 16, 2013

Vijana Jazz 'Wana Saga Rhumba' wafufuka na 3 mpya


                Wanamuziki wa Vijana Jazz Band wakiwa mazoezi katika ukumbi wa Vijana Social

Wanamuziki wa Vijana Jazz Band wakiwa mazoezi katika ukumbi wa Vijana Social

BENDI ya muziki wa dansi iliyowahi kutamba zamani, Vijana Jazz 'Wana Saga Rhumba' imeanza kujipanga upya kwa kunyakua wanamuziki wapya na kufyatua nyimbo tatu mpya.
Nyimbo hizo ambazo mmoja umeshatolewa video yake ni pamoja na 'Wanawake Wanaweza' wenye video, 'Mtanieleza Nini' na 'Mwanangu Njoo Nikuusie'.'
Katibu wa bendi hiyo, Mgonahazeru, aliiambia MICHARAZO nyimbo hizo tatu zimetungwa na yeye, Saburi Athuman na muimbaji wao mpya waliyemnyakua toka Tango Stars, Julius Mwesiwe.
"Baada ya kupata vyombo vipya, Vijana Jazz tumeanza kujipanga upya kurejesha makali yetu kwa kuwanyakua wanamuziki wapya na kufyatua nyimbo tatu mpya ikiwemo wenye video," alisema.
Alisema nyimbo iliyotolewa video ni 'Wanawake Wanaweza' ambao ameutunga yeye, huku nyimbo zilizosalia zikiwa mbioni kufanyiwa hivyo huku wakijiandaa kuanza kufanya maonyesho.
Mgonahazeru alisema mbali na Mwesiwe, Vijana Jazz iliyowahi kutamba na nyimbo kadhaa kama Nimeruka Ukuta, Maria, Bujumbura, Shoga, Mpiga Debe na vingine pia imewanyakua wanamuziki wengine wawili.
Wanamuziki hao ni muimbaji wa zamani wa Mchinga Soudn, Roshy Mselela na Hussein Bomu aliyewaji kuwika na UDA Jazz.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...