Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, May 11, 2013

FAINALI YA POOL KWA VYUO VIKUU KUFANYIKA MOROGORO MEI 11 Meneja Mauzo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wa Mkoa wa Morogoro, Jemes Gomile(kushoto) akimkabidhi Vifaa vya michezo,Nahodha wa timu ya Chuo cha SUA, Calvin Mjema wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Vyo shiriki vya mashindano ya mchezo wa Pool kwa Vyuo vya Elimu ya juu Mkoani Morogoro.Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Morogoro, Patrick Lugang’ha.

Na Mwandishi Wetu, Morogoro
KAIMU Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, John Laswai  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya mchezo wa Pool 'Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013'. kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoa wa Morogoro yatakayofanyika Mei 11. 
Akizungumza na waandishi wa habari jana  wakati wa kukabidhi sare za kuchezea pamoja na fedha kwa ajili nauli na maadalizi kwa vyuo vitakavyoshiriki, mwenyekiti wa chama cha mchezo huo mkoani hapa (MOPA), Patrick Lugeng'ha alisema kuwa mashindano hayo yatakayoshirikisha vyuo vikuu vinne yatafanyikia kwenye ukumbi wa Vijana.
Lugeng'ha alisema kuwa mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager yatafunguliwa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa na yatafungwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro,Lydia Mbiaji.
Aliongeza kwa kuvitaja vyuo vitakavyoshiriki mashindano hayo kuwa ni chuo cha SUA, Mzumbe, Ardhi na chuo cha uandishaji wa habari (  MSJ).
Lugeng'ha alisema kuwa mashindano hayo yatachezwa kwa mtindo wa chuo kwa chuo na mchezaji mmoja mmoja wanaume na wanawake.
Alisema bingwa kwa upande wa chuo licha ya kujinyakulia fedha taslim Sh.500,000 pia itakuwa imekata tiketi ya kuuwakilisha mkoa huo katika fainali za taifa zitakazofanyika kuanzia Juni mosi mwaka huu jijini Dar es Salaam, mshindi wa pili atazawadiwa Sh.300,000, mshindi wa tatu Sh.200,000 na mshindi wa nne Sh.100,000.
Aidha alisema kuwa bingwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) atajinyakulia Sh.150,000 na tiketi ya kushiriki fainali za taifa, mshindi wa pili Sh.100,000, ambapo bingwa kwa upande wa wanawake atazawadiwa Sh.100,000 na tiketi ya kushiriki fainali za taifa huku mshindi wa pili akiondoka na Sh.50,000.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...