Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 29, 2013

The Finest’ ya Mwana FA yapisha msiba wa Ngwea


Na Elizabeth John

MKALI wa muziki wa bongo fleva nchini, Mwana FA amesema ameahirisha kufanya shoo yake ambayo inajulikana kwa jina la ‘The finest’ ambayo ilitakiwa kufanyika leo, ili kuupisha msiba wa msanii wa hip hop nchini, Albert Mangwea uliotokea Mei 28 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwana FA alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na umuhimu wa msanii huyo katika tasnia ya muziki wa hip hop nchini.
Mbali na Mwana FA, wasanii wengine ambao wamesogeza mbele na kuhairisha kufanya shoo zao ni pamoja na Lady Jay Dee, Izzo Business, Joeh Makini na Kalapina.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...