Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 30, 2012

TBL YASHINDA TUZO YA USALAMA MAHALA PA KAZI SEKTA YA VIWANDA


Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kushoto), akimkabidhi tuzo Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda, baada ya kampuni hiyo kushinda masuala ya usalama mahali pa kazi, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama kazini duniani, Dar es Salaam juzi. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Makongoro Mahanga.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kulia) akimpongeza , Renatus Nyanda kwa niaba ya TBL.
Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Kabaka pamoja na baadhi ya washindi wa tuzo hizo.

TRA YAPUNGUZA KODI YA BODABODA


Venance George, Morogoro
MAMLAKA ya Mapato (TRA) mkoani Morogoro, imewapunguzia kodi wafanyabishara ya pikipiki maarufu kama bodaboda kutoka Sh95,000 hadi Sh35,000 kwa mwaka kwa pikipiki moja.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na kaimu Meneja wa mamlaka hiyo mkoani hapa, Kilomba Kanse na kuthibitishwa na Meneja wa Mkoa, Hakim Kimungu, hatua hiyo imefikiwa na mamlaka kufutia ombi la wafanyabishara hao kutaka kupunguziwa kodi hiyo.

Kimungu alisema kuwa wafanyabishara hao kupitia chama cha waendesha pikipiki mkoani Morogoro (CCWPM) waliwasilisha maombi kwenye mamlaka hiyo wakitaka kupunguziwa kodi na kutoa sababu kuwa idadi ya pikipiki mkoani Morogoro imeongezeka huku idadi ya wateja ikiendelea kuwa ile ile, hali ambayo imedaiwa kupunguza mapato yao.

“Sisi sababu hiyo tuliiona kuwa ni ya msingi, kwa vile mkoa wa Morogoro kwa sasa unapikipiki nyingi kuliko pengine mikoa yote ukiachilia mkoa wa Dar es Salaam, ongezeko hilo limesababisha idadi ya wateja kupungua na kupungua kwa mapato yao,” alisema Meneja huyo.

Aliongeza kuwa TRA mkoa wa Morogoro imekuwa na mazungumzo na mwenyekiti wa CCWPM, Anamwikira Massawe, na kufikia makubaliano hayo na kwamba hatua hiyo ilizingatia vigezo vya mamlaka hiyo ambapo walipakodi kama wafanyabiashara ya bodaboda miaka mitatu iliyopita walikadiriwa kulipa kodi ya Sh95,000 kutokana na kipato chao kufikia kati ya Sh3 milioni na Sh7 milioni kwa mwaka.

Alisema kutokana na ongezeko la pikipiki mapato ya wafanyabishara hiyo yameonekana kushuka mpaka kufikia chini ya Sh3 milioni kwa mwaka kiwango ambacho kinaipa mamlaka uwezo kuwatoza Sh35,000 kwa mwaka, kiwango ambacho ni cha chini kwa walipakodi wa kukadiriwa wasiofanya mahesabu.

Kimungu alisema kuwa punguzo hilo la kodi litakuwa ni kwa wafanyabishara wa bodaboda wote mkoani Morogoro, lakini alisisitiza kwamba wenye pikipiki nyingi zaidi ya moja watatozwa kulingana na makadirio ya faida ya mapato yao kwa mwaka.

“Pamoja na punguzo hilo la kodi TRA tutaendelea kufanya uchunguzi wetu kwa njia mbalimbali na pale ambapo tutajiridhisha kuwa mapato ya waendesha pikipiki hao yameongezeka tena tutarudi kuwatoza kiasi kile kile cha Sh95,000 kwa mwaka na wale wenye pikipiki nyingi tumeanza kuwalazimisha kufanya mahesabu ili watozwe kodi kulingana na hesabu hizo,” alisema.

Hata hivyo kwa mujibu wa barua ya mamlaka hiyo ya kujibu ombi la bodaboda imeeleza kuwa bodaboda ambao wamekwisha kadriwa kwa kulipa Sh95,000 kwa mwaka huu watalipa punguzo la kodi hiyo mwakani lakini ambao hawajakadiriwa na hawajalipa kodi hiyo watalipa kodi mpya ya Sh35,000 kodi ambayo itaanza kutozwa April 27, 2012.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa CCWPM, aliipongeza mamlaka hiyo kwa hatua ya kuwapunguzia kodi na kuongeza kuwa uamuzi huo utawafanya bodaboda kwenda kulipa kodi kwa hiari badala ilivyokuwa mwanzo ambapo wengine walikuwa wakilipa kodi kwa kusukumwa.

Massawe amewataka waendesha pikipiki mkoa wa Morogoro kushirikiana na mamlaka ya mapato ili kodi mpya iliyopendekezwa iweze kukusanywa kwa urahisi na kwamba hatua hiyo pia itaiwezesha mamlaka kukuzanya mapato zaidi kwa kuwa walipa kodi hiyo wataweza kuongezeka. Chanzo; Mwananchi

NHIF YAANZISHA KLABU YA MAZOEZI KWA WATUMISHI WAKE KILA J'MOSI KWENYE VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI OYSTERBAY



 

 Wafanyakazi wa mfuko wa bima wa afya NHIF wakiwa mazoezini katika viwanja vya shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es salaam.
Hapa wakifanya mazoezi ya kukimbia kuzunguka uwanja wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es salaam. 


Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya wajiandaa na uzinduzi wa klabu ya michezo kwa watumishi wake ili kuwapa fursa ya kulinda afya zao na magonjwa mabalimbali yanayotokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha ya kila siku kama vile kisukari, shinikizo la damu na mengineyo mengi ambayo kwa kwa sasa yamekuwa tishio kwa maisha ya binadamu wa leo.
 
Akizungumza wakati wa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Oyesterbay Meneja wa timu ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha rasilimali watu na utawala bi Jane nchimbi alisema 'Tumekuwa na utaratibu huu tangu mwanzoni mwa mwaka jana lakini kidogo tulikuwa tumebanwa na majukumu ,lakini kwa sasa tumeamua kwa pamoja kuufanya utaratibu huu kuwa endelevu kwani utasaidia kujenga afya hasa ikizingatiwa kuwa watumishi wengi wa umma  tunatumia muda mwingi kwenye ofisini tukihudumia wateja hivyo kuwa na nafasi finyu kushiriki mazoezi kama ambavyo NHIF tumethubutu...
Mpango huu unawajumuhisha pia wale watumishi wa Mfuko kwenye ofisi  za Mkoani, mpango wa baadaye ni kuwa na eneo maalum la kufanyia mazoezi (Gym) ili huduma zote za msingi ziweze kupatikana.alisema Bi Jane kijazi
 
Naye nahodha wa timu ya mpira wa pete  ya NHIF bi Sabina Komba  ……aliwataka wafanyakazi wanaoshiriki mazoezi kwenye klabu hiyo kutambua kuwa wao ni mabalozi katika kuhamasisha wananchi na wananchama wa mfuko huo kupenda na kuthamini michezo kwani mfumo wa maisha ya kisasa umegubikwa na maradhi mengi na  makubwa ambayo yanaathiri afya zetu na walio wengi

MASHINDANO YA 10 BORA WA MASUMBWI KUFANYIKA MAY 4



Na Mwandshi Wetu


MASHINDANO ya kumi bora ya mchezo wa masumbwi yanatarajia kufanyika mei 4 katika ukumbi wa

Panandi Panandi Ilala Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa kimataifa

wa mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' alisema vijana wengi wamejitokeza kushiriki

michuano hiyo yenye lengo la kupanga viwango vya mabondia.

Aliwataja baadhi ya mabondia watakaopambana siku hiyo ni Ibrahim Class atakaezichapa na Idi

Mnyeke, Amiri Macho atazidunda na West Scorpion,Charo Issa na Hamis Nassoro,Athumani Sadara

na Abuu Mtambwe, Hassan Mijugu ataoneshana kazi na Saidi Ally, Sandari Nyambara na Pascal

Ignus.

Pamoja na mapambano mengine yatakayokuwa katika uzito tofauti tofauti vijana wengi

wamejitokeza hivyo tunaomba sapoti ya aina yoyote kutoka kwa wadau wa mchezo wa masumbwi

kufanikisha mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kinyogoli Fondition kwa ajili ya kuwapanga

katika viwango mbalimbali vya ubora wa wachezaji,

Alitaja baadhi ya maitaji kwa siku hiyo ni kuwa maji kwa wachezaji wakati wakiwa

ulingoni,zawadi za kuwatia moyo wachezaji pamoja na madawa mbalimbali yatakayotumika kwa

ajili ya kuwapatia mabondia huduma ya kwanza alisema Super D.

Kwa yoyote mwenye nia ya kusaidi mashindano hayo kwa namna moja au nyingine anaweza

kuwasiliana
na kocha
Mkongwe Habibu Kinyogoli kwa namba ya simu 0655928298 au unaweza fika katika klabu

ya Amana CCM iliyopo Ilala Dar es Salaam vilevile waweza
kuwasiliana na kocha Super D

0713/0787-406938 au unaweza fika Klabu ya Ashanti Iliyopo Ilala Soko la Mitumba kwa mawasiliano zaidi

Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
kwa Mawasiliani zaidi ya mtandao

Sunday, April 29, 2012

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA MPAMBANO WA CHEKA NA MAUGO

 Baadhi ya Maraisi wa vyama vya mchezo wa Masumbwi Nchini wakiangalia mchezo wa Mada Maugo na Francis Cheka ubingwa wa IBF AFRIKA kutoka kushoto ni Rais wa TPBO,Onesmo Ngowi wa TPBC pamoja na Emanuel Mlundwa wa PSTwww.superdboxingcoach,blogspot.com

 Ibrahimu Maokola kulia akipambana na Saidi Mbelwa Maokola alishinda kwa Point.Picha na www.superdboxingcoach,blwww.superdboxingcoach,blogspot.comogspot.com

Baadhi ya Marefarii kutoka Nnje ya nchi wakisubili kuchezasha mpambano wa ubingwa wa IBF Arika kati ya Mada Maugo na Francis Cheka jana.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya mashabiki waliokuwa wamekaa katika VIP wakiangalia mpambano
Mada maugo kushoto na Francis Cheka wakioneshana umwamba wa kutupiana masumbwiwww.superdboxingcoach,blogspot.com

Cheka akipiga ngumi bila mafanikio uku mada akiludi nyuma kujiami.www.superdboxingcoach,blogspot.com
Meya wa Manspaa ya Ilala Jery Slaa akimkabidhi funguo ya gari bondia Francis Cheka baada ya kuibuka na ubingwa wa k.o raundi ya 6 jana.www.superdboxingcoach,blogspot.com

KAIMU MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AZUNGUMZIA USAFI JIJINI



Kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Mwamtum Mahiza akiongea na
waandishi wa habari jana Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuhusu hali
ya usafi katika jiji la Dar es salaam ambayo imekuwa hairidhishi kwa
muda mrefu hali hiyo imesababishwa na wananchi kutozingatia kanuni
sheria na taratibu za afya na usafi wa mazingira.

(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE).

TANGAZO LA DAWA YENYE NGUVU




DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI
ALLY WA YANGA BOMBA UHURU NA MSIMBAZI 0787230551 AU 0652755838


PIGA NO O713827689, 0755074505 , au 0719 541366
,0652755838 UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM

BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884

SHULE YA UHURU FIKA JENGO LA AZAM BAKHRESA ULIZA NGAEJA 0715110900

KARIAKOO SHULE YA UHURU STENDI YA MABASI YA TANDIKA ULIZIA ZUNGU MUHUZA TIKETI 0712743870

NA UKIWA ILALA SHARIF SHAMBA FIKA DSJ BANDA NAMBA 14 SIMU 0718718671

NA UKIWA KOTA ZA BANDARI KARIAKOO FIKA MKUNGUNI KIBANDANI KWA HUSEIN 0753893295

MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU ULIZA MACHELLAH 0713470492

ENZOY INALETA HESHIMA
You might also like:

SIMBA KUIVAA AL AHLY SHANDY YA SUDAN LEO UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM.


Wawakilishi pekee waliobaki toka Klabu za Tanzania katika michuano ya Barani Afrika, Simba, leo wanatinga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya michuano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa kucheza na Al Ahly Shandy ya Sudan.

Katika Raundi zilizopita, Simba walibwaga Kiyovu ya Rwanda kwa jumla mabao 3-2 katika Mechi mbili kisha kuwatoa ES Setif ya Algeria kwa bao la ugenini baada ya kufungana bao 3-3 katika Mechi mbili, Simba wakishinda Dar es Salaam bao 2-0 na kuchapwa 3-1 huko Mjini Setif, Algeria.

Nao Al Ahly Shandy waliwatoa Ferroviario de Maputo ya Msumbiji Raundi iliyopita na ingawa Klabu hii ya Sudan ni mara ya kwanza kucheza michuano ya Klabu Afrika lakini kwa mchezo ilioonyesha walipocheza na Ferroviario de Maputo na kushinda 1-0 ugenini Maputo na 2-0 kwenye Mechi ya marudiano, Timu hii si ya kubeza.

Timu hizi zitarudiana hapo Jumamosi Mei 12 huko Mjini Shandy, Mji ambao uko Kilomita 150 Kaskazini Mashariki ya Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum.

Na katika mechi hiyo kiingilio cha chini ni sh 5,000/=

RAIS KIKWETE AWA MWENYEJI WA MKUTANO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ARUSHA


Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakitia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngordoto jijini Arusha. 
Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakionesha hati baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngordoto jijini Arusha.  
 Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikaribishwa chakula cha mchana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Richard Sezibera baada ya picha ya pamoja kufuatia kutia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngordoto jijini Arusha

CHEKA AGALAGAZA MAUGO BILA URUMA


MAUGO ADUNDWA NA CHEKA


BONDIA Francis Cheka ‘SMG’ kutoka Morogoro, kwa mara ya tatu mfululizo Jana Usiku amempiga mpinzani wake Mada Maugo kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba katika pambano lililokuwa la raundi 12, kwenye ukumbi wa PTA, Saba Saba, Dar es Salaam.
Maugo baada ya kupigwa ngumi nyingi katika raundi tatu mfululizo, kiasi cha kutabiriwa kukaa chini wakati wowote, mwanzoni mwa raundi ya saba hakurejea ulingoni.
Msaidizi wake, Karama Nyilawila alitupa taulo ulingoni akisema bondia wake hataendelea na pambano.
Refa John Shipanuka kutoka Zambia aliyelimudu pambano hilo, alimuinua mkono Cheka kumtangaza mshindi kwa TKO raundi ya saba.
Baada ya hapo, Maugo aliinuka kwenye kona yake na kwenda kumkumbatia Cheka na kocha wake, akisema kwamba amesalimu amri baada ya kuishiwa pumzi.
“Pumzi imekata, siwezi kuendelea,”alisema Maugo ambaye leo alionekana muungwana ingawa hakuwa tayari kusema atahitaji pambano la nne au la.
Akiwa mwenye furaha, Cheka alisema kwamba anamshukuru Mungu amemuwezesha kuendeleza ubabe wake kwa mabondia wa Tanzania na sasa anageuzia makali yake kwa Japhet Kaseba ambaye naye ameomba pambano la marudiano.
Katika pambano la jana, refa Shipanuka alimdhibitu Maugo mwenye desturi ya kuwakumbatia wapinzani wake ili kukwepa kupigwa na pia kupumzikia kwenye miili yao.
Kila alipokuwa akimkumbatia Cheka, Shipanuka alikuwa akifika na kuwaachanisha na kufanya mabondia hao watumie muda mwingi kupigana.
Pamoja na hayo, Maugo alilianza pambano hilo vizuri na katika raundi ya pili almanusra ashinde kwa Knockout (KO) baada ya kumkalisha mpinzani wake kwa ngumi kali.
Lakini SMG aliinuka na kuendelea na pambano, ingawa limchukua hadi raundi ya nne kuanza kuutawala mchezo.
Raundi ya kwanza hadi ya tatu, Maugo alifanya vizuri, lakini baada ya hapo mambo yalikuwa magumu na tangu hapo wengi walijua angepigwa wakati wowote.
Katika  mapambano ya utangulizi, mdogo wake Cheka, Cosmass Cheka alipigwa kwa pointi na Sadiki Momba katika pambano la uzito wa Light, wakati Hajji Juma alimpiga kwa pointi Emmilio Naffat uzito wa bantam.
Simba Watunduru alimpiga kwa KO raundi ya sita Mohamed Kashinde katika pambano la uzito wa Feather, wakati Amos Mwamakala alimpiga kwa pointi Said Muhiddin uzito wa Light.

Moro Best alimpiga Nassib Ramadhan kwa TKO raundi ya nne uzito wa Bantam na Salima Kabombora alimpiga Asha Ngedere kwa pointi uzito wa Bantam.

TIGO YAZAMINI MAADHIMISHO YA SIKU YA TAALUMA VYUO VIKUU MAKUMBUSHO

Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Leon Haule (kulia) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu umuhimu wa Social Protection wakati wa maadhimisho ya siku ya Taaluma kwa Vyuo vikuu liliyofanyika Makumbusho ya Taifa kwa udhamini wa Tigo
Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Josephine Douglas(kulia) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu umuhimu wa Social Protection wakati wa maadhimisho ya siku ya Taaluma kwa Vyuo vikuu liliyofanyika Makumbusho ya Taifa kwa udhamini wa Tigo

Mwenekiti wa Bodi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Charles Nyoni (katikati) akikata utepe wakazi wa ziara ya kuzungukia vibanda vya maonyesho wakati wa maadhimisho ya siku ya Taaluma kwa Vyuo vikuu liliyofanyika Makumbusho ya Taifa kwa udhamini wa Tigo.Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha IFM, Profesa Mjema na Mwanafunzi wa Chuo hicho, Dorthea Msofe.

Tigo yawezesha wakazi wa Muheza

. Mmmoja wa washindi aliyejishindia zawadi ya simu kutoka Tigo
Kikundi cha Sarakasi kikipagawisha mashabiki waliofurika kwenye Tamasha la Tigo wilayani Muheza hivi karibuni.
Mwanamuziki H.Baba akiwaburudisha wakazi wa Muheza

GARI LAMTOKEA PUANI MADA MAUGO BAPINGWA KWA K,O RAUNDI YA 7



 Bondia Francis Cheka (kulia) akimsukumia konde mpinzani wake Mada Maugo, wakati wa pambano lao lililokuwa la Raundi 12 lililofanyika katika Ukumbi wa PTA usiku huu. Mada Maugo aliwashangaza mashabiki wa mchezo huo pale alipoanza pambano hilo kwa spidi ya ajabu na kufanikiwa kumpeleka chini mpinzani wake mara mbili katika raundi ya pili na ya tatu, baada ya raundi ya nne mchezo ulibadilika na Mada kuanza kuelemewa na kupoteza mwelekeo huku akikumbatia kila mara.
Ilipofika raundi ya sita kabla ya kuanza raundi ya saba, Mada Maugo alitangaza kutoendelea na mchezo kwa kile alichodai kuishiwa na pumzi huku akisikika kusema, 'Sirudi Jamaa ataniua' huku akivua Glovz na kumpa ushindi mpinzani wake wa Teknical Know Count TKO.
Baada ya mchezo huo alipohojiwa na mtandao huu Mada alisema kuwa ilipofika raundi ya nne tu alikuwa hamuoni mpinzani wake jukwaani lakini alijikaza na kuendelea kushambulia huku akishtukia makonde yanatua usoni na ndipo ilipofika raundi ya sita aliamua kumwambia msimamizi wake kuwa hawezi kuendelea na pambano hilo.
 Mada Maugo, akimpeleka chini mpinzani wake Cheka.
 Mashabiki wa Mada, wakishangilia...
 Mada Maugo (kulia) akishambulia kwa konde zito.
 Wakichapana kwa zamu...
 Mada akishambulia....
 Mashabiki wa ngumi wakishangilia pambano hilo.
 Mashabiki wa Cheka, wakishangilia na kulizunguka gari alilokabidhiwa Cheka, baada ya kutangazwa mshindi.
 Cheka akisaidiwa na polisi baada ya kuzongwa na mashabiki wake wakitaka kumbeba na kuzunguka naye ukumbini humo baada ya kushinda pambano hilo.
 Nasib Ramadhan (kushoto) akichapana na Moro Best katika moja ya pambano la utangulizi, ambapo Nasib alishinda kwa KO katika Raundi ya nne.
 Simba wa Tunduru (kulia) akishangilia baada ya kumchapa mpinzani wake Mohamed Kashinde kwa KO katika Raundi ya 6 Dakika ya 2 na Sekunde 59, huku mohamed akiwa naongoza kwa mchezo bomba kabla ya kuangushwa.
 Simba wa Tunduru, akishangilia kwa staili yake baada ya kumwangusha mpinzani wake.
 Mgeni Rasmi, Meya wa Ilala, Jerry Slaa, akiwa na baadhi ya viongozi wa mchezo huo meza kuu wakifuatilia kwa makini mapambano hayo.
 Mrembo, Elizabeth Pertty, akipita jukwaani kuonyesha namba za raundi ya pambano hilo.
Cosmas Cheka (kulia) akipambana na Sadick Momba. Katika pambano hilo Momba alishinda kwa Pointi
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...