Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 30, 2012

MASHINDANO YA 10 BORA WA MASUMBWI KUFANYIKA MAY 4Na Mwandshi Wetu


MASHINDANO ya kumi bora ya mchezo wa masumbwi yanatarajia kufanyika mei 4 katika ukumbi wa

Panandi Panandi Ilala Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa kimataifa

wa mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' alisema vijana wengi wamejitokeza kushiriki

michuano hiyo yenye lengo la kupanga viwango vya mabondia.

Aliwataja baadhi ya mabondia watakaopambana siku hiyo ni Ibrahim Class atakaezichapa na Idi

Mnyeke, Amiri Macho atazidunda na West Scorpion,Charo Issa na Hamis Nassoro,Athumani Sadara

na Abuu Mtambwe, Hassan Mijugu ataoneshana kazi na Saidi Ally, Sandari Nyambara na Pascal

Ignus.

Pamoja na mapambano mengine yatakayokuwa katika uzito tofauti tofauti vijana wengi

wamejitokeza hivyo tunaomba sapoti ya aina yoyote kutoka kwa wadau wa mchezo wa masumbwi

kufanikisha mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kinyogoli Fondition kwa ajili ya kuwapanga

katika viwango mbalimbali vya ubora wa wachezaji,

Alitaja baadhi ya maitaji kwa siku hiyo ni kuwa maji kwa wachezaji wakati wakiwa

ulingoni,zawadi za kuwatia moyo wachezaji pamoja na madawa mbalimbali yatakayotumika kwa

ajili ya kuwapatia mabondia huduma ya kwanza alisema Super D.

Kwa yoyote mwenye nia ya kusaidi mashindano hayo kwa namna moja au nyingine anaweza

kuwasiliana
na kocha
Mkongwe Habibu Kinyogoli kwa namba ya simu 0655928298 au unaweza fika katika klabu

ya Amana CCM iliyopo Ilala Dar es Salaam vilevile waweza
kuwasiliana na kocha Super D

0713/0787-406938 au unaweza fika Klabu ya Ashanti Iliyopo Ilala Soko la Mitumba kwa mawasiliano zaidi

Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
kwa Mawasiliani zaidi ya mtandao

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...