Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 19, 2012

ZIARA YA RAIS DK ALI MOHAMED SHEIN HUKO WETE-PEMBARais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akizungumza na
Viongozi wa Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba, katika mkutano wa
majumuisho ya ziara aliyoifanya katika Wilaya hizo zilizo katika Mkoa
wa Kaskazini Pemba, iliyomalizika jana kwa mkutano huo ulifanyika
katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,(kushoto) katibu Mkuu
Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee na Waziri wa Bishara,Viwanda na
Masoko Nassor Ahmed Mazrui. [Picha na Ramadhan Othma,Pemba.]
Baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Wete na
Micheweni Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na Viongozi
hao katika mkutano wa majumuisho ya ziara aliyoifanya katika Wilaya
hizo zilizo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, iliyomalizika jana kwa
mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
Wete.[Picha na Ramadhan Othma,Pemba.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
Msikiti Masjid Raudha,katika kijiji cha Kiuyu Maungweni Jimbo la
Ole,Mkoa wa Kaskazini Pemba jana,alipofanya ziara katika Kijiji hicho.
[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj
Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Watoto mara baada ya kuzindua
Msikiti Masjid Raudha katika shehia ya Kiuyu Maungweni,pamoja na
kuzungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Shehia hiyo jana,katika
jimbo la Ole Mkoa wa Kaskazini Pemba.[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiwasalimia waumini wa Dini ya Kiislamu
baada ya kuzungumza na kuwapa nazaha zake wakati uzinduzi wa Msikiti
Masjid Raudha,katika kijiji cha Kiuyu Maungweni Jimbo la Ole,Mkoa wa
Kaskazini Pemba jana,alipofanya ziara katika Kijiji hicho. [Picha na
Ramadhan Othman,Pemba.]

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...