Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 18, 2012

SIMBA YAIKANDAMIZA JKT RUVU 3-0 UWANJA WA TAIFA, YANGA YACHAPWA KAITABA


Mchezaji Uhuru Selemani wa timu ya Simba kushoto akishangilia goli la kwanza alilofunga dhidi ya timu ya JKT Ruvu pamoja na na wachezaji wenzake Gervas Kago kulia na Patrick Mafisango, Simba imecheza na JKT Ruvu kwenye uwanja wa Taifa jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ambapo Simba imeshinda magoli 3-0 yakifungwa na wachezaji Uhuru Selemani mwenyewe,Haruna Moshi "Boban", na Mwinyi Kazimoto.Mchezo wa leo umeisogeza zaidi Simba kuelekea kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Vodacom Bara.


Wakati huohuo timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam imeangukia pua tena huko Bukoba Mkoani Kagera baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 kwenye uwanja wa Kaitaba jioni ya leo.
Mashabiki wa Timu ya Simba wakishangilia kwa nguvu baada ya timu yao kujipatia magoli dakika za mwanzomwanzo za mchezo huo.
Hiki ndicho Kikosi cha JKT Ruvu kikiwa katika picha ya pamoja.
picha nahttp://www.fullshangweblog.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...