Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 25, 2012

MKURUGENZI MANISPAA YA ILALA AKANUSHA KUSIMAMISHA MIKATABA YA MGAMBOMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala amekanusha taarifa zilizozagaa mitaani kuwa halmashauri hiyo imesimamisha mikataba ya mgambo wa wilaya hiyo na kuingia mkataba na Kampuni binafsi ambayo ingeanza kazi Mei Mosi mwaka huu.
 
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Gabriel Fuime wakati  alipokuwa akizungumza na Fullshangweblog  jijini Dar es Salaaam jana kuhusu uvumi huo kuwa hauna ukweli wowote.
Alisema Halmashauri haijafikia uamuzi huo bali kinachofanyika hivi sasa ni kuangalia nama iliobora katika usimamizi wakazi zinazofanywa na mgambo hao ambapo kama kutakuwa na ulazima kazi hiyo watakabidhiwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
“Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa jeshi la mgambo halitendi kazi zake kwa kufuata sheria kwamba wamekuwa wakijihusisha zaidi na vitendo vya rushwa”alisema Fuime
Fuimea alisema ndio maana wamo katika upembuzi yakinifu ili ikiwezekana wawape jeshi kazi hiyo kwa kuamini kuwa wataifanya katika kiwango bora ukilinganisha na hivi sasa.
Alisema vikao kuhusu mipango ya kuboresha huduma hiyo vinafanyika na wakati ukifika itatolewa hadharani na kila mmoja wenu atajua lakini kwa sasa hatujawasimamisha mgambo hao ambapo wanaendelea na kazi kama kawaida.
Aidha, mgambo hao wamekuwa wakifanyakazi kwa mkataba wa miezi mitatu ambapo mara wamalizapo huomba mkataba tena bila ya kuwa na uhakika wakufanikiwa.
Fuime alisema mgambo hao hulipwa posho ya ujira kwa siku ndani ya mwezi mmoja kiasi cha shilingi 120,000.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...