Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, April 17, 2012

Rais akutana na Viongozi waliosimamia zao la karafuu Wete Pemba


Jumla ya shs Billioni 71 wamejipatia Wakulima wa Zao la Karafuu Kisiwani Pemba baada ya kuliuzia Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) Karafuu zao zao katika msimu wa Karafuu unaotarajiwa kumalizika hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ameyaeleza hayo leo hapo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi alipokuwa akitowa shukrani kwa Viongozi mbali mbali wa Mkoa huo wakiwamo vikosi vya ulinzi vya Polisi, JKU,KMKM,,ZIMAMOTO,VALANTIA, MAFUNZO,MASHEHA, WANANCHI NA KIKOSI KAZI CHA TAIFA CHA USIMAMIZI WA ZAO LA KARAFUU ZANZIBAR.
Amesema kuwa kiasi hicho cha Fedha kimo mikononi mwa Wananchi ambapo kwa kiasi kikubwa zinaweza kuwasaidia sana katika maendeleo yao.
Dkt Shein amefurahishwa na juhudi mbali mbali mbali za Maendleo zinazochukuliwa na Wakulima kwa kuweza kujenga Nyumba za Kisasa baada yakupata Fedha hizo za Karafuu ambapo pia amewataka kuchukuwa kila juhudi yakusafisha Mashamba yao na kupanda Mikarafuu mipya.
Aidha Dkt Shein amefurahishwa na juhudi ya pamoja ziliochukuliwa na Viongozi mbali mbali, Wananchi, Masheha pamoja na Vikosi vya Ulinzi katika kuhakikisha kuwa msimu huu zao la Karafuu halitoroshwi kwa njia ya Magendo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...