Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 15, 2012

Mama yake Kanumba atoa wosia kwa SHIWATA

Na Peter Mwenda

MAMA Mzazi wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba amewataka wasanii wanachama wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kuendeleza ushirikiano alioacha mwanae.

Akizungumza katika ibada ya kumuombea mwanae iliyoandaliwa na M (SHIWATA) leo Dar es Salaam, Mama Kanumba alisema amefarijika kuona wasanii wanaendelea kumuombea mwanae kila kona ya nchi.

"Nawashukuru SHIWATA kwa moyo wa ipendo na ushirikiano mlionesha kwa familia yangu, naomba muendeleze ushirikiano mliokuwa nao wakati mwanangu akiwa nanyi, endeleeni kushirikiana" alisema Mama Kanumba.

Katika ibada hiyo iliyoongozwa na mchungaji wa Kanisa la Elim Pentekoste Ilala Bungoni, Mchungaji Livingstone Mwaitela alisema wasanii na familia ya Kanumba wasisononeke kwa sababu Mungu alimpenda mtoto wao huyo zaidi.

Alisema wasanii waendelee kumkumbuka mwenzao kwa kubadili mambo yasiyompendeza Mungu badala yake wajiandae kwa kufanya mambo ambayo yanampendezesha na kujiweka tayari siku akiwaita wawe tayari.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Caasim Taalib alisema Kanumba alikuwa mwanachama wao namba 648 akiwa mmoja wa waliojitokeza kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga nyumba za wasanii kutoka Bagamoyo, Kisarawe na hatimaye kufanikiwa kupata eneo Mkuranga.

Marehemu Kanumba alifariki Aprili 5, wakati akikimbizwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuanguka nyumbani kwake Sinza kufuatia ugomvi wa mapenzi na msanii mwenzake Elizabeth Michael (Lulu).

1 comment:

  1. Binafsi nakupongeza kwa kazi nzuri ya kuelimisha jamii.na kwa kutupatia habari motomoto,leo ndo nimefungua blog yako kwa mara ya kwanza ila nitaendele kuwa mwanachama hai wa hii blog.
    Kila la kheri katika ujenzi wa Taifa

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...