Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 26, 2012

Odama Achanganya wanaume Leaders!MSANII maarufu kwenye tasnia ya filamu nchini, Jenifer Kyaka ‘Odama’ Jumapili iliyopita aliwachanga wanaume kwenye Viwanja vya Leaders, Dar es Salaam kutokana na kubadilika kila mara.

Midume iliyokuwa ikitwanga starehe kwenye viwanja hivyo maarufu jijini Dar es Salaam, ilijikuta ikimfuatilia bila matumaini baada ya dada huyo kubadilika-badilika .

"Huyu dada sijui vipi mara ya kwanza alionekana kavalia nguo nyingine, mda tena tunamuona na vazi jingine niyeye huyu ama ," alisikika akisema kidume mmoja.

Hata hivyo hali hiyo pia ilishuhudiwa pia na wadau wengine ambao walisema huenda
Odama yuko kwenye maandalizi ya filamu hivyo anafanya mazoezi.

Kwani mda wa saa 6:00 alionekana kavaa vazi la dela na wakati giza likianza kuingia katika viwanja hivyo, ghafla tena akaonekana kuvaa fulana na suruali yenye kubana 'taiti'.

Msanii huyo hivi karibuni ameanzisha kampuni yake ya iitwayo J-Film 4 Live kwa ajili ya kazi hizo za tasnia hiyo ya filamu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...