Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 22, 2012

ZIARA YA KATIBU MKUU KIONGOZI ALIPOTEMBELEA JENGO LA BUNGE MJINI DODOMA JANA Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah, (wa pili kushoto) akimuongoza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, wakati akiingia mjengoni Bungeni kwa Waheshimiwa Wabunge. Balozi Sefue jana alifanya ziara ya kutembelea jengo hilo la Bunge.
 Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah akimuonesha katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue sehemu za kukaa maofisa wa Serikali ndani ya Ukumbi wa Bunge kipindi wawapo ndani ya ukumbi huo kusikiliza hoja mbalimbali zinazohusu Wizara zao.
  Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah akimuonesha katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue mtambo wa kudhibiti vipaza sauti pamoja na picha za video Bungeni.
 Mtaalamu wa mitambo ya Sauti na Picha kutoka Ofisi ya Bunge, Lemo Toluwe, akimpa maelezo Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ya namna mitambo hiyo inavyofanya kazi Bungeni.
  Mhandisi wa umeme kutoka Wakala wa Majengo wa Seriikali, Hijja Mrutu, akitoa maelezo juu ya namna mitambo ya kufua Umeme Bungeni inavyofanya kazi.
 . Patson Sobha 'MCHUNGAJI' kutoka Idara ya Hansard, Bungeni akitoa maelezo kwa Balozi Sefue ya namna Hansard inavyoandaliwa baada ya kunasa sauti za majadiliano Bungeni.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akifurahia mitambo ya kisasa ya kunasa picha za matukio yote katika viwanja vya Bunge.
Naibu waziri wa Miundombinu Mhe. Harrison Mwakyembe, akimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue walipo kutana Bungeni juzi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...